'Unafanya hendisheki nasi tuende wapi,'Mashabiki wamuuliza Octopizzo baada ya kumpongeza Khaligraph

Rappa Octopizzo Jumanne aliwashangaza wengi baada ya kuamua kuweka ugomvi wake kando kati wa mwenzake Khaligraph Jones, huku akimuandikia ujumbe wa kumpongeza baada ya kuchaguliwa katika tuzo la BET.

Katika ujumbe wake Octopizzo aliwauliza mashabiki wake waweze kumpigia kura Jones ili aweze kuleta tuzo nyumbani,rappa huyo alisisitiza kuwa ugomvi wao utabaki vile ilhali anamtakia memo yote.

"Tumekuwa na tofauti zetu na ugomvi wetu na hilo litabaki vivyo hivyo.lakini hongera Brayo Kjones kwa tuzo lako, mashabiki wangu mpigieni kura Jones 

na akishinda hiyo award namvutisha vela cha lazima si at nini." Aliandika Octopizzo.

Baadhi ya mashabiki wake walifurahishwa na ujumbe wake huku wengi wakumuuliza watakwenda wapi kama ata weka ugombi wao kando na kuleta amani kati yao.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

Kevin Fitness: Unafanya Handshake ndio sisi tuende Wapi?

dania ya twita: Rada rada chafu Octo unadrip mbaya, tuangushie ngoma bana umelala siku kathaa

cally: Octo the king ligi yako in ya kina Shakur

 bluesman kenya: Naona Sasa umeanza kupata akili. Lakini mambo ya vela tuache mihadarati. Kichwa ndogo can't accommodate both bangi na akili.Choose wisely