'Niko tayari kuenda nyumbani,'Sonko asema huku hoja ya kumfurusha ikiwasilishwa

Muhtasari
  • Gavana Sonko asema kuwa yuko tayari kuenda nyumbani hii ni baada ya hoja ya kumfurusha kuwasilishwa na wawakilishi wadi
sonko
sonko

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesisitiza kwamba hayuko tayari kutia saini ili kuachili fedha za kaunti kwa NMS.

Awali Sonko kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook alisema kwamba kuna maisha baada ya siasa na hatokubali kutishiwa maisha na mtu yeyote.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Sonko alisema baba yake hakuwa mwanasiasa na yuko tayari kuenda nyumbani.

 
 

Usemi wake unajiri saa chache baada ya wawakilishi wadi kuwasilisha hoja ya kumfurusha ofisini gavana huyo.

Mwanasiasa huyo alisema kwamba atasimama kidete kama seneti walipokuwa na mjadalai kuhusu mswada wa mapato wa kaunti yake.

"Si hitaji kuokolewa, nitasimama kidete kama seneti walipokuwa wanshughulikia mswada wa mapato ya kaunti 

Sitaki,sitaenda na sitaenda kupeana saini yangu ili kuachilia fedha kwa taasisi isiyo halali." Aliandika Sonko.

Maneno yake yalijiri alipokuwa anamjibu mmoja wa wana mitandao alipouliza haswa ni nani ataenda kumuokoa baada ya hoja ya kumfurusha kuwasilishwa.

Sonko aliendelea na kusema kwamba;

"Niko tayari kuenda nyumbani,nilisema awali kuwa kuna maisha baada ya siasa baba yangu hakuwa mwanasiasa."