Isiolo: Wanawake 3, wanaume 2 na mtoto wauliwa kwenye mashambulizi ya kigaidi

Gavana kuti amesema kuwa mgogoro wa mipaka kati ya Isiolo na upande wa Kaskazini Mashariki unahitaji kusuluhishwa ili kumaliza mashambulizi.

Muhtasari

•Magaidi ambao wanaaminika kutoka kaunti jirani ya Wajir waliua wanawake watatu, wanaume wawili na mtoto mmoja katika kijiji cha Mado Wale kilicha kaunti ndogo Merti, Isiolo.

•Punde baada ya hayo magaidi hao waliharibu kisima cha maji kilichokuwa katika kijiji hicho.

Crime scene
Crime scene

Watu sita walipoteza maisha yao kwenye uvamizi wa kigaidi kaunti ya Isiolo.

Magaidi ambao wanaaminika kutoka kaunti jirani ya Wajir waliua wanawake watatu, wanaume wawili na mtoto mmoja katika kijiji cha Mado Wale kilicha kaunti ndogo Merti, Isiolo.

Punde baada ya hayo magaidi hao waliharibu kisima cha maji kilichokuwa katika kijiji hicho.

Maafisa wa polisi wanafikishwa katika maeneo yaliyoathirika ili kutafuta na kukamata waliotekeleza uhalifu huo.

Imeripotiwa kuwa kando na mauaji, hakuna chochote wavamizi hao  walichoiba kwani waliuwa na kutoweka.

Gavana wa Isiolo, Mohammed Kuti amelaani kitendo hicho na kuagiza maafisa wa usalama kufanya hara kutafutana na magaidi hao ili haki itendeke.

Hata hivyo, nia ya magaidi hao haijabainishwa ila gavana Kuti amesema kuwa huenda inahusiana na mgogoro wa mipaka.

"Tunaomba serikali kufanya hara kukamata washukiwa kabla hakujaharibika zaidi"Kuti alisema.

Alisema kuwa mgogoro wa mipaka kati ya Isiolo na upande wa Kaskazini Mashariki unahitaji kusuluhishwa ili kumaliza mashambulizi.