'Alikuwa anauliza kuhusu watoto,'Mkewe askari aliyeuawa na Kangogo,asema askari huyo alikuwa anampigia simu

Muhtasari
  • Mke wa John anasema Caroline alimpigia simu kila mara kumchunguza, hii ilikuwa mwezi mmoja kabla ya kifo cha mumewe
  • Juliet Ogweno alizungumza na runinga ya  Citizen alisema kwamba hakushuku kuwa wawili hao walikuwa wapenzi wakati huo

Askari jambazi Caroline Kangogo anatafutwa na polisi. Amekuwa mafichoni kwa siku 7 sasa kwa mauaji  ya polisi Constable John Ogweno na mshauri wa usalama Peter Ndwiga.

Mke wa mwathiriwa wake wa kwanza wa mauaji ameelezea jinsi Caroline alikuwa  maishani mwake.

Mke wa John anasema Caroline alimpigia simu kila mara kumchunguza, hii ilikuwa mwezi mmoja kabla ya kifo cha mumewe.

Juliet Ogweno alizungumza na runinga ya  Citizen alisema kwamba hakushuku kuwa wawili hao walikuwa wapenzi wakati huo.

Alisema pia kwamba Caroline alikuwa akitaka sana watoto wa John wapelekwe Nakuru kuwatembelea na kukaa nao.

"Kila wakati akipiga simu alikuwa anauliza kuhusu watoto, wako aje? Mnaendelea aje? Nataka siku moja John akuje awachukue akuje nao Nakuru wajienjoy . . . vitu kama hizo,"Juliet alieleza.

Mke na watoto wa marehemu Ogeno wanaishi Kasupul Kabondo, Homabay.

Siku tatu kabla ya John kupigwa risasi na kuuawa, Caroline aliwasiliana na Juliet na kumhakikishia kuwamumewe amefika salama huko Kericho na ameenda kazini moja kwa moja.

Katika hali ya kusikitisha, Jumamosi, Julai 3,  2021 kabla ya kifo chake, Caroline alimpigia simu Juliet kumwambia, John amethibitisha kuwa ataweza kuhudhuria mahafali ya watoto ambayo yamewekwa kwa leo (Jumamosi, Julai 10, 2021).

"Alhamisi, Julai 1, alinipigia simu kunieleza kuwa John alikuwa amefika Kericho. John alikuwa ameenda kazi

Kisha Jumamosi, Julai 3 kisha alinipigia na kunieleza kuwa John atakuja sherehe ya watoto iliyokuwa ifanyike Julai 10

Hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo ya mwisho kati yangu naye," Alizungumza JUliet.