Trans-Nzoia:Mwanamke auguza majeraha baada ya kupigwa risasi na jamaa akifikiri ni Kangogo

Muhtasari
  • Mwanamke auguza majeraha baada ya kupigwa risasi na jamaa akifikiri ni Kangogo
  • Baada ya kisa hicho, Muyundo aliripoti suala hilo kwa polisi katika Kituo cha Polisi cha Kiminini akisema alifyatua risasi ili kumtisha
Caroline Kangogo

Mwanamke anauguza majeraha ya risasi baada ya jamaa mmoja kumpiga risasi akisema alifikiri ni afisa anayesakwa Caroline Kangogo.

Phanice Chemutai Juma alipigwa risasi ya tumbo na Ken Muyundo Alhamisi usiku katika soko la Kiminini, kaunti ya Trans Nzoia.

Baada ya kisa hicho, Muyundo aliripoti suala hilo kwa polisi katika Kituo cha Polisi cha Kiminini akisema alifyatua risasi ili kumtisha.

Mfanyibiashara huyo, aliripoti tukio hilo saa tatu unusu usiku. Aliwaambia maafisa kwamba alidhani Chemutai alikuwa  polisi wa kike, Caroline Kangogo.

Muyundo alidai mwathiriwa huyo alikuwa akimpigia simu bila kukoma iliwapatane na kudai kwamba hawajuani.

Lakini Chemutai ambaye anapokea matibabu  katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kitale alisema walikutana na kubadilishana namba a simu hapo awali.

Muyundo yuko mikononi mwa polisi akihojiwa kuhusu kisa hicho.

Polisi wamepata bastola l Ceska, jarida lililobeba risasi kumi na katriji iliyotumika, zote ni za Muyundo.

Kangogo anatafutwa kwa mauaji ya wanaume wawili; polisi John Ogweno na mfanyabiashara wa Juja Peter Ndwiga.