Polisi Wachunguza Chanzo cha Mkasa wa Moto Nyumbani kwa Mutahi Ngunyi

Muhtasari
  • Polisi Wachunguza Chanzo cha Mkasa wa Moto Nyumbani kwa Mutahi Ngunyi
Nyumba ya Mutahi Nguyi iliyotekezwa na moto Runda
Image: HISANI

Mchambuzi wa kisiasa Mutahi Ngunyi ameandika taarifa na polisi juu ya moto uliyotokea nyumbani kwake Runda Jumatano.

Kamanda wa mkoa wa Nairobi Augustine Nthumbi alisema Ngunyi alienda katika kituo cha polisi kilicho karibu ili kurekodi taarifa hiyo.

" Maafisa wa polisi wanachunguza kilichosababisha mkasa wa moto nyumbani kwa mchanganuzi Mutahi Ngunyi, tunataka kujua ni kwa nini na ni nani alisababisha moto huu," Nthumbi alisema.

Nthumbi alisema kulikuwa na watu watatu ndani ya nyumba hiyo.

"Mutahi, mkewe na mfanyikazi wao walikuwa ndani ya nyumba wakati moto ulizuka lakini wote walitoroka bila kuumia," alisema.

Nyumba ya Mutahi iliteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana huko Runda.

Nyumba hiyo kubwa iliwaka moto wakati moshi mweusi ulipofukia kutoka kwenye makazi karibu saa 1.45 asubuhi.

Wazima moto kutoka kaunti za Kiambu na Nairobi walifanikiwa kuzima moto mwendo wasaa kumi alfajiri.

"Nyumba yangu ya Runda ya miaka 27 iliteketea mwendo wa saa saba na dakika 45 asubuhi. Itumbi, uliambia Hustlers mwendo wa saa nane na dakika moja asubuhi takriban dakika 16 baadaye kuwa ni baada ya kuzungumzia ghasia za Kiambaa za mwaka 2008 kwenye 5th Estate," liandika Ngunyi.