STORI ZA GHOST

Jamaa anayedai kuwa na ujuzi wa kutengeneza ndege akamatwa akiwa amevalia mavazi ya kike Lamu

Mutahi Wahome, 35,alikuwa amevalia buibui, sidiria na chupi ya kike huku akiwa amebeba mkoba mkononi.

Muhtasari

•Alipoulizwa sababu zake kupatikana akitembea nje licha ya masaa ya amri ya kutotoka nje kutimia, Wahome alisema kuwa alikuwa anashughulikia mabawa kwani anajaribu kuboresha ujuzi wake wa kupaa.

•Aliwaarifu polisi kuwa anaamini kuwa alikuwa amerogwa kwani amekuwa akivalia mavazi ya kike tangu akiwa na umri wa miaka tisa.

Mutahi Wahome akiwa amevalia buibui katika kituo cha polisi cha Lamu
Mutahi Wahome akiwa amevalia buibui katika kituo cha polisi cha Lamu
Image: CHETI PRAXIDES

Polisi walimkamata mwanaume mmoja aliyepatikana akiwa amevalia mavazi ya kike katika maeneo ya Bajuri kwenye kisiwa cha Lamu usiku wa Jumamosi.

Mutahi Wahome, 35,alikuwa amevalia buibui, sidiria na chupi ya kike huku akiwa amebeba mkoba mkononi.

Alipoulizwa sababu zake kupatikana akitembea nje licha ya masaa ya amri ya kutotoka nje kutimia, Wahome alisema kuwa alikuwa anashughulikia mabawa ya ndege kwani anajaribu kuboresha ujuzi wake wa kuendesha ndege.

Alisema kuwa anakusudia kupaa kutoka Dunia na  kuenda mpaka kwa Sayari zingine.

Wahome alisema kuwa ana maarifa mengi ya kutumika kwenye sekta ya sayansi ya vyombo vya anga na akadai kuwa yuko karibu kupata kibali cha kumruhusu kupaa angani ya nchi bila kuzuiawa na yeyote.

Jamaa huyo alisema kuwa anapendelea kufanya mazoezi ya kupaa ufukoni mida ya usiku kwani pale kuna hali nzuri ya mazoezi.

"Sitaki kusababisha ajali. Ndio maana nafanya mazoezi wakati ambapo hakuna watu. Tena ufukoni kuna upepo ambao hunisaidia kujaribu kasi ya mabawa yangu. Kama tu kwenye uvumbuzi mwingine, huwezi fanya majaribio mahali ambapo kuna watu ijapokuwa unajiamini" Wahome alisema.

Wahome alikimbizwa na polisi wakati alipatikana akizurura nje usiku. Polisi walisema kuwa walitilia shaka kasi kubwa ya 'mwanamke' huyo ila wakaja kugundua kuwa ni mwanaume.

Alipofikishwa kituoni, jamaa huyo alivuliwa mavazina kutambulikana kuwa mwanaume aliyevalia mavazi ya kike.

Aliwaarifu polisi kuwa anaamini kuwa alikuwa amerogwa kwani amekuwa akivalia mavazi ya kike tangu akiwa na umri wa miaka tisa.

Wahome ambaye alihamia Lamu kutoka Nyeri mwaka uliopita amekuwa akifanya kazi katika duka moja la useremala  lililo Mkomani ambako amedai kuwa akifanyia uvumbuzi wake anapoendelea kujitatarisha kupaa.

(Utafiri; Samuel Maina)