Kumshinda Ruto ndicho kipaumbele changu - Kalonzo asema

Kalonzo alieleza imani yake katika kutwaa ushindi wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022

Muhtasari

•Kalonzo pia aliwaomba Wakenya kupuuzilia mbali mfumo wa uchumi wa naibu rais wa kutoka chini kwenda juu akisema kuwa huwa ni mpango tu wake kurudi mamlakani.

•Pia alikanusha madai kuwa ameshiriki mkutano na kinara wa ODM Raila Odinga ili kuzuia chama cha Wiper kujiondoa kutoka muungano wa NASA.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka
Image: LINAH MUSANGI

Aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka amemwambia naibu rais William Ruto awe tayari kwa ushindani mukubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kwani lengo lake kuu ni kumshinda.

Kalonzo alieleza imani yake katika kutwaa ushindi wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

"Kushinda Ruto ndilo jambo napatia  kipaumbele na najua kwa nini. Pia namkaribisha ndugu yangu Johnson Muthama kufanya kazi nasi tupate ushindi kwani kuwashinda ni lazima" Kalonzo alisema.

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi maeneo ya Mwingi ya kati siku ya Jumamosi, kiongozi huyo wa Wiper alisema kuwa jamii ya Wakamba imetengwa sana kwa muda na wakati umefika waunge mkono mmoja wao ashinde kiti cha urais," Alisema.

Kalonzo pia aliwaomba Wakenya kupuuzilia mbali mfumo wa uchumi wa naibu rais wa kutoka chini kwenda juu akisema kuwa huwa ni mpango tu wake kurudi mamlakani.

"Kama ni suala la kuwa hasla, basi nadhani jamii yetu imekabliwa na changamoto nyingi na tunajua 'hustling' ni nini" Aliendelea kusema.

Alisema kuwa viongozi wote wako huru kufika pembe zote za nchikuuza sera zao bila ya kujalisha wanaoshirikiana nao kisiasa.

Pia alikanusha madai kuwa ameshiriki mkutano na kinara wa ODM Raila Odinga ili kuzuia chama cha Wiper kujiondoa kutoka muungano wa NASA.

Kalonzo alisema kuwa hakuna sababu zitakazopelekea uchaguzi mkuu wa mwaka uja kusongeshwa mbele na kusema kuwa sababu tu inaweza kusababisha hali hiyo ni ikiwa kuna vita nchini.

Viongozi wengine ambao walihudhuria hafla hiyo ni pamoja na mbunge wa Kitui Irene Kasalu, Mbunge wa Mwingi ya kati Gideon Mulyungi, aliyekuwa seneta wa Kitui David Musila, aliyekuwa seneta wa Kakamega Bonnie Khalwale na mwenyekiti wa UDA Johnston Muthama kati ya wengine.

(Utafsiri; Samuel Maina)