Mike Sonko kutoa zawadi ya elfu 200,000 kwa mtu atakayetoa habari itakayosababisha kukamatwa kwa Wanjala

Muhtasari
  • Mike Sonko kutoa zawadi ya elfu 200,000 kwa mtu atakaye toa habari itakayo sababisha kukamatwa kwa Wanjala

Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko ameahidi, kutoa zawadi ya elfu mia mbili kwa mtu yeyote atakayetoa habari itakayo sababisha kukamatwa kwa mtuhumiwa Wanjala.

Mnamo siku ya Jumatano Marten Wanjala alikimbia kutoka kituo cha polisi kwa ni isiyojulikana.

Polisi wanasema alikuwa anatarajiwa mahakamani leo na kwamba kusakwa kwake kunaendelea.

Muuaji wa 'Vampire' aliyekiri kutekeleza mauaji hayo alifungwa kwa siku 30 ili polisi kuchunguza zaidi mauaji ya watoto nane.Polisi walisema idadi ya waathirika huenda ikawa ni 13.

Wanjala alikuwa mbele ya hakimu mkuu wa Makadara Angello Kithinji wakati polisi walisema walihitaji muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi.

Mtuhumiwa huyo alikiri kwamba, ametekeleza mauaji hayo, huku akiwapaeleka wapelelezi na polisi eneo la uhalifu huo.

Je mtuhumiwa huyo ametoweka aje, ilhali alikuwa mikononi mwa polisi?ni swali ambalo wananchi wanajiuliza baada ya kusikia habari za kutoweka kwa Wanjala.

"Mtuhumiwa wa mauaji ya watoto Masten Wanjalla ametoroka kutoka kituo cha polisi cha Jogoo. Ninatoa zawadi ya Kshs. 200,000 / = kwa mtu yeyote ambaye atatoa habari ambayo itasababisha kukamatwa kwa mnyama huyu na polisi," Aliandika Sonko.