Mtangazaji wa Radio Jambo Mzee Toldo ahitaji msaada wa matibabu

Muhtasari

•Familia ya mtangazaji huyo wa soka imesema kwamba anahitaji kufanyiwa operesheni ya kubadilisha figo kwa dharura ili kurejesha afya yake.

Mtangazaji Toldo Kuria
Mtangazaji Toldo Kuria
Image: FACEBOOK

Mtangazaji wa kipindi cha Weekend Warm Up kwenye Radio Jambo John Kuria Mwangi almaarufu kama Mzee Toldo ametoa ombi la kuchangisha shilingi milioni 4.5 ili kugharamia matibabu yake nchini Uturuki.

Mzee Toldo ambaye hivi majuzi aligundulika kuwa na tatizo la figo  ameomba wasamaria wema kumsaidia kuchangisha kiasi hicho ili aweze kusafiri hadi Uturuki kupandikizwa figo.

Familia ya mtangazaji huyo wa soka imesema kwamba anahitaji kufanyiwa upasuaji kubadilishiwa figo kwa dharura ili kumrejeshea afya yake.

"Hivi majuzi mwana wetu, baba, kaka, rafiki aligunduliwa kuwa na tatizo la figo na anahitaji upandikizaji wa haraka wa figo. Hii itafanyika nchini Uturuki. Gharama ya jumla ya operesheni ni shilingi milioni 4.5. Kwa hivyo tunaomba msaada wako wa kifedha kusaidia familia kupata pesa zinazohitajika ili kumwezesha  kupata matibabu ya haraka na kukidhi gharama" Familia ya Toldo imesema.

Mtangazaji huyo ameomba Wakenya kusimama naye kwa kumsaidia kwa kiasi chochote kile watakachoweza kupitia Paybill 8044929, ACC (weka jina lako).

Image: TOLDO KURYA

"Tafadhali simama nami katika kipindi hiki cha majaribu, nahitaji kusimama tena kwa miguu yangu na kukimbia. Tafadhali nisaidieni nipate matibabu. "chochote kile mungu atakujalia nitashukuru" "Hakuna tendo la fadhili, hata liwe dogo jinsi gani, halipotei kamwe." Toldo amesema.

Mchango wako utathaminiwa sana tunapoendelea kumtakia mtangazaji wetu mpendwa afueni ya haraka.

MHARIRI DAVIS OJIAMBO