Wanafunzi wa Molo Wafikishwa Mahakamani Kwa Biashara ya Kusafirisha Bangi Shuleni

Wanafunzi hao wawili walitiwa nguvuni Jumanne

Muhtasari

•Wanafunzi wawili wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Njenga Karume katika kaunti ndogo ya Molo  wapewa kifungo cha miezi sita baada ya hakimu Wangari Kamau kuwapata na hatia ya kukutwa na bangi shuleni.


Mahakama
Mahakama

Wanafunzi wawili wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari Njenga Karume katika kaunti ndogo ya Molo  wapewa kifungo cha miezi sita baada ya hakimu Wangari Kamau kuwapata na hatia ya kukutwa na bangi shuleni.

Wanafunzi hao wenye umri wa miaka 16 na 17 walinaswa kufuatia taarifa iliyoashiria kuwa walikuwa wamebeba dawa hiyo shuleni na walikuwa na nia ya kuisambaza kwa wanafunzi wengine.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 anayeaminika kuwa nyuma ya genge la biashara haramu alikamatwa akiwa na roli nne, huku mshirika wake akikamatwa pia.

Maafisa wa upelelezi katika mji huo wako katika hali ya tahadhari baada ya ripoti za kijasusi kuashiria kwamba vijana wanaosoma shule wameingizwa katika kundi la ulanguzi wa dawa za kulevya, wakiongozwa na mshukiwa maarufu ambaye amejificha.

Wanafunzi hao wawili walitiwa nguvuni Jumanne baada ya kupatikana na misokoto ya bhangi.

Ripoti za matumizi ya bhangi nchini zimeongezeka mara dufu katika siku za hivi karibuni haswa kutokana na mgombea urais wa chama cha Roots, wakili msomi profesa George Wajackoyah kutangaza kwamba moja kati ya ajenda kuu za manifesto yake ni kusukuma uhalalishwaji na bhangi nchini ili kupika jeki zoezi za kulipa deni la kitaifa ambalo kwa sasa lipo zaidi ya trilioni 9 pesa za Kenya, taifa la Uchina likiwa limeongoza katika kutoa mikopo ya kufadhili miundo msingi humu nchini.