Matokeo ya KCPE kutangazwa leo kutoka saa tano

Muhtasari

•Watahiniwa wataweza kuangalia matokeo yao kutumia simu kwa kutuma nambari ya usajili kwa 20076.

Waziri wa Elimu George Magoha akihutubia wanahabari Kisumu mnamo Machi 21, 2022.
Waziri wa Elimu George Magoha akihutubia wanahabari Kisumu mnamo Machi 21, 2022.
Image: FAITH MATETE

Hatima ya watahiniwa milioni 1.2 waliofanya mtihani wao wa KCPE 2021 hivi majuzi itajulikana leo mwendo wa saa tano.

Kwa sasa waziri wa elimu Fred Matiang'i anatoa taarifa kwa rais Uhuru Kenyatta.

Watahiniwa wataweza kuangalia matokeo yao kutumia simu kwa kutuma nambari ya usajili kwa 20076.

Mwaka huu KNEC ilisajili watahiniwa 1,225,507 katika vituo 28,316 vya mtihani wa KCPE ikilinganishwa na watahiniwa 1,191,752 katika vituo 28,467 mwaka wa 2020.

Mtihani wa KCPE 2021 ulifanyika kati ya Machi 7 na Machi 9.

Mengine yatafuata...