Polisi Uganda wamtia mbaroni Bobi wine kwa saa,8, na kuwachapa wanahabari

Muhtasari
  • Bobi Wine atiwa mbaroni kwa muda wa saa,8, huku wanahabari wakipokea kichapo cha mbwa kutoka kwa polisi
  • Akiwa kwenye mahojiano Bobi Wine alisema kwamba ameponea kifo mara mbiki kwa muda wa wiki mbili

Unyanyasaji na ukatili wa polisi umezidi kushuhudiwa nchini Uganda mbele ya uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka wa 2021.

Mwaniajai kiti cha urais aliyekuwa msanii nchini humo Bobi Wine amepokea mateso huku baada ya kutiwa mbaroni na polisi alilazimika kukaa kwenye gari kwa saa 8.

Mnamo Desemba,12 National Unity Platform (NUP) bwalijawa na hasira nyingi baada ya polisi kuendeleza ukatili wao.

Pia polisi hao waliwapa wanahabari kichapo cha mbwa huku wengine wakisalia na majeraha kutokana na kichapo hicho.

Awali akiwa kwenye mahojiano Bobi Wine alisema kwaba ameponea vifo mara mbili.

" Nimeponea kifo mara mbili kwa muda wa wiki mbili iliyopita, nimekuwa nikifyatuliwa risasi kila ninapokwenda kwenye kampeni, inanilazimu nivalie bullet proof ili kuepuka majeruhi ya risasi, gari langu limefyatulia risasi kwenye gurudumu, vyioo zangu zimepasuliwa lakini najua hii ni siasa, tutashinda vita." Alisema Bobi Wine.