Fahamu kwanini Wanajeshi wa Marekani wakati wa kunyongwa kwa Saddam Hussein

Bardenwerper anakiri kwamba wakati alipomkabidhi Saddam kwa wale waliokua wanakaribia kumnyonga, wanajeshi wote waliokuwa wanamlinda walikuwa na machozi machoni mwao.

Muhtasari

•Wanajeshi kumi na wawili waliokuwa wametumwa kumlinda Saddam Hussein hawakuwa marafiki bora zaidi wa Saddam Hussein bali pia marafiki zake wa mwisho aliokuwa nao

•Bardenwerper ananukuu mmoja wa wanajeshi wenzake, Adam Rogerson, akisema, 'Hatukuwahi kumuona Saddam kama muuaji katili . Alionekana kama babu yetu.

•Saddam alimwambia askari mwingine kwamba iwapo nitaruhusiwa kutumia pesa zangu. Niko tayari kulipa ada ya elimu ya chuo ya mtoto wako wa kiume.

Image: GETTY IMAGES

Wanajeshi kumi na wawili waliokuwa wametumwa kumlinda Saddam Hussein hawakuwa marafiki bora zaidi wa Saddam Hussein bali pia marafiki zake wa mwisho aliokuwa nao.

Wanajeshi hawa, walichaguliwa kutoka miongoni mwa polisi 551 wa Kampuni ya kikosi cha polisi, ambao walikuwa na Saddam hadi muda wake wa mwisho, waliitwa 'Super Twelve'.

Mmoja wao, Will Bardenwerper, ameandika kitabu 'Mfungwa ndani ya kasri lake, Walinzi wake wa Kimarekani na Kile ambacho historia ilikiacha bila kusema' , 'The Prisoner in His Palace, His American Guards , and What History Left Unsaid' ambapo alielezea maelezo ya kina kuhusu kilichotokea siku za mwisho walipokuwa wakimlinda Saddam.

Bardenwerper anakiri kwamba wakati alipomkabidhi Saddam kwa wale waliokua wanakaribia kumnyonga, wanajeshi wote waliokuwa wanamlinda walikuwa na machozi machoni mwao.

'Saddam alionekana kama babu'

Bardenwerper ananukuu mmoja wa wanajeshi wenzake, Adam Rogerson, akisema, 'Hatukuwahi kumuona Saddam kama muuaji katili . Alionekana kama babu yetu.

Saddam alishitakiwa mahakamani kwa kuamuru mauaji ya wapinzani wake 148.

Will Bardenwerper alikuwa miongoni mwa kundi la wanajeshi 12 wa Marekani waliokuwa wakimlinda Saddam Hussein
Will Bardenwerper alikuwa miongoni mwa kundi la wanajeshi 12 wa Marekani waliokuwa wakimlinda Saddam Hussein
Image: GETTY IMAGES

Siku za mwisho za maisha yake aliishi gerezani Iraqi akisikiliza nyimbo za mwanamuziki wa Marekani Mary J. Blige. Alipenda kuendesha baiskeli yake ya mazoezi ya mwili, ambayo alikuwa akiita 'Pony'.

Alikuwa anapenda sana kula pipi na alikuwa anatamani sana kula keki ndogo aina ya Muffin.

Bardenwerper aliandika kwamba katika siku zake za mwisho mienendo na tabia zake kwa watu wale ilikuwa ya adabu sana na hakuonesha kwamba aliwahi kuwa kiongozi katili sana wakati wa utawala wake.

Castro alinifundisha kuvuta sigara

Saddam alipenda sana kuvuta sigara aina ya 'Cohiba', ambazo alizitunza katika kijisanduku cha karatasi zenye unyevunyevu za (wet wipes). Alikuwa anasema kuwa miaka iliyopita, Fidel Castro alikuwa amenifundisha kuvuta sigara.

Image: GETTY IMAGES

Bardenwerper ameeleza kwamba Saddam alipenda sana kutengeneza bustani na alikuwa akipenda hata kupalilia na kukitengeneza kichaka kilichokuwa kinaota katika mazingira ya gereza na kukifanya kama maua.

Saddam alikuwa mwangalifu sana kuhusu chakula chake

Alikuwa anatengeneza kifungua kinywa chake kwa awamu. Kwanza mayai ya kukaangwa, halafu keki na mwisho matunda. Iwapo mayai ya kukaangwa yalionekana kukatika katika vipande basi alikuwa anakataa kuyala.

Bardenwerper anakumbuka kwamba wakati mmoja Bw Saddam alielezea ukatili uliofanywa na mwanae wa kiume Uday, ambao ulimuudhi sana Saddam.

Fudel Castro na Saddam Hussein
Fudel Castro na Saddam Hussein
Image: GETTY IMAGES

Kile kilichotokea iilikuwa ni kwamba Uday alikuwa amefyatua risasi kwenye umati wa watu waliokuwa katika sherehe, ambapo watu wengi waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa.

Saddam alikasirika sana kutokana na hilo kiasi kwamba aliagiza magari yote ya Uday yateketezwe kwa moto.

Saddam mwenyewe alicheka alipokuwa akituambia alivyochoma magari ya gharama kubwa ya Uday kama vile Rolls-Royce, Ferrari na Porsche na kushuhudia miale ya moto ikitoka kwenye magari hayo.

Mwanajeshi wa Marekani aliyehusika katika ulinzi wa Saddam alimwambia kwamba kaka yake amefariki. Aliposikia taarifa hii Saddam alimkumbatia na , akamwambia 'Kuanzia leo unichukulie kama kaka yako.'

Saddam alimwambia askari mwingine kwamba iwapo nitaruhusiwa kutumia pesa zangu. Niko tayari kulipa ada ya elimu ya chuo ya mtoto wako wa kiume.

Saddam Hussein
Saddam Hussein
Image: POOL

Usiku mmoja kila mtu alimuona mwanajeshi mwenye umri wa miaka, Dawson, akitembea huku akiwa amevalia suti kubwa kuliko umbo lake. Ilibainika kuwa Saddam alikuwa amempatia Dawson suti yake kama zawadi.

Bardenwerper ameandika kwamba, 'Kwa siku kadhaa tulimcheka Dawson, kwasababu alikuwa anavaa suti ile na kutembea kana kwamba alikuwa anatembea kwenye onyesho la 'mitindo ya mavazi' .'

Urafiki uliendelea kushamiri baina ya Saddam na walinzi waliokuwa wakimlinda, ingawa walikuwa na maagizo ya wazi ya kutojaribu kuwa karibu na Saddam kabisa.

Hussain aliiishi katika magereza mawili wakati wa kesi yake.

Mojawapo ya vyumba vya Mahakama ya Kimataifa mjini Baghdad, na maeneo mengine yalikuwa ni kasri zake zilizokuwa kaskazini mwa Baghdad, majengo ambayo yalikuwa katika kisiwa, yaliyoweza kufikiwa kwa kutumia daraja tu.

Bardenwerper ameandika, 'Hatukumpatia Saddam zaidi ya alichostahili. Lakini hatukuumiza utu wake..

Steve Hutchinson, Chris Tasker na walinzi wengine walijaribu kubadilisha chumba cha duka kuwa ofisi ya Saddam.

Mpango ulipangwa kumshangaza Saddam

Meza ndogo na kiti cha ngozi viliondolewa kwenye chumba na kuweka bendera ndogo ya Iraqi

Image: GETTY IMAGES

Saddam Hussein alikamatwa na askari wa Marekani alipokuwa amjejificha.

Bardenwerper anaandika, 'Lengo la yote haya ilikuwa ni kujaribu kutengeneza mazingira ya gereza yafanane na ya ofisi ya kiongozi wa serikali kwa ajili ya Saddam. Mara tu alipoingia kwenye chumba hicho kwa mara ya kwanza , askari alikimbia haraka kwenye meza na kufuta vumbi.

Saddam aliona ishara hii na kutabasamu wakati akikaa kwenye kiti

Huu ni wakati Saddam Hussein alipokamatwa na wanajeshi wa Marekani
Huu ni wakati Saddam Hussein alipokamatwa na wanajeshi wa Marekani
Image: GETTY IMAGES

Saddam alikuwa anakaa kwenye kiti kila siku na askari waliokuwa wanamlinda walikaa kwenye viti wakitazamana

Saddam alitengenezewa Mazingira kama vile mahakama ni yake.

Bardenwerper anafafanua kwamba askari walijaribu kwa uwezo wao kumfanya Saddam awe na furaha. Kwa upande wa Saddam yeye alikuwa anacheka na kutaniana naye na kufanya mazingira hayo kuwa ya furaha.

Baadae baadhi ya askari walimwambia Bardenwerper walikuwa wanaona kwamba kama jambo lolote baya lingewatokea, basi Saddam angeweza kuhatarisha maisha yake kwa ajili yao'

Kila wakati Saddam alipopata nafasi, alikuwa akiwaomba askari kumlinda pamoja na familia yake.

Sehemu iliyowashangaza wengi kwenye kitabu hiki ni ile ambayo, inaelezwa kuwa askari hao waliomboleza kifo cha Saddam, wakati wakichukuliwa kama maadui wakubwa wa Marekani.

Adam Rogerson, mmoja wa askari hawa alimueleza Will Bardenwerper kwamba 'baada ya Saddam kunyongwa, tuliona kama tumemsaliti.

Tulijiona kama sie ndio wauaji wake. uilijiona tumemuua mtu ambaye alikuwa karibu yetu.

Baada ya Saddam kunyongwa, mwili wake ulitolewa nje, umati uliokuwepo nje walimtemea mate na kumdhihaki.

Askari wa Marekani walipigwa na butwaa

Bardenwerper anaandika baada ya kuona hivyo, askari hao 12 waliokuwa wanamlinda Saddam mpaka umauti wake walipigwa na butwaa.

Mmoja wao alijaribu hata kusalimiana kwa mikono na umati uliokuwepo, lakini wenzake walimkataza.

Mmoja wa askari hawa, Steve Hutchinson, alijiuzulu nafasi yake ndani ya jeshi la Marekani baada ya Saddam kunyongwa.

Hutchinson alikuwa anajishughulisha na shughuli za kufundisha matumizi ya bunduki huko Georgia mpaka kufikia mwaka 2017.

Anajivunia pia kitendo cha kutakiwa kutojihusisha na Wairaqi ambao walikuwa wanaudhihaki mwili wa Saddam Hussein.

Saddam alikuwa anamatumaini mpaka siku zake za mwisho kwamba asingenyongwa.

Mwanajeshi akibeba picha ya Saddam Hussein
Mwanajeshi akibeba picha ya Saddam Hussein
Image: ROMEO CANCAD

Askari, Adam Rogerson, alimwambia Bardenwerper kwamba Saddam aliwahi kumwmabia kwamba angeingia kwenye uhusiano na mwanamke, kwamba atakapotoka jela ataingia kwenye ndoa ingine.

Disemba 30, 2006, Saddam Hussein aliamshwa alfajiri ya saa tisa usiku.

Akaambiwa kwamba anakwenda kunyongwa muda mfupi ujao. Baada ya kupokea ujumbe huo, alioga taratibu na kujiandaa kwa ajili ya kunyongwa.

Hofu yake wakati huo ilikuwa, 'Je Askari wale 12 walikuwa wamelala?'

Dakika chache kabla ya kunyongwa, Saddam alimuita Steve Hutchinson aliyekuwa nje ya seli yake na kumpatia saa yake aina ya 'Raymond Weil'.

Hutchinson alipotaka kukataa, Saddam alimlazimisha kupokea. Mpaka leo, saa hiyo inafanya kazi kwenye nyumba ya Hutchinson huko Georgia.