Paka mkongwe duniani asherehekewa kwa kufikisha miaka 27

Paka huyo mwenye jina Flossie alizaliwa mwaka wa 1995

Muhtasari

• Flossie na mmiliki wake aitwaye Vicki  wanaishi pamoja jimbo la Orpington huko London.

• Alichukuliwa na kulelewa na Vickie Green baada ya wamiliki wao wa kwanza kufa.

Paka mzee duniani ana umri wa miaka 27
Paka mzee duniani ana umri wa miaka 27
Image: Guinness World Records

Rekodi za Dunia za Guinness zimezua gumzo kote duniani baada ya kuripoti kuwa kuna paka anayeitwa Flossie mwenye umri wa miaka 27 kuwa ndiye paka mwenye umri mkubwa zaidi duniani.

Paka huyo anaripotiwa alizaliwa mwaka wa 1995 miaka sawa na mwanamume anayemmiliki aitwaye Vicki Green alimchukua paka huyo na kumlea tangu mwaka wa 2022 alimpomchukua kutoka kwa washikadau wa kulinda paka wa eneo hilo.

Hapo awali, Paka huyo, Flossie miaka mitatu baada ya kuchukuliwa na Vicki alikuwa anaishi wa wamiliki wengine baada yao kufa na baadaye kushauriwa na daktari wa wanyama wamchukue na kumlea.

Flossie (Paka huyo) na Vicki sasa wanaishi pamoja Orpington huko London.

Kulingana na Vicki paka huyo ingawaje ni mzee sana ni kiziwi na anapenda sana kubembelezwa na kula chakula.

Vicki akisimulia kwa furaha kwenye video ya Guinness world Book of Records alisema "Nilijua tangu mwanzo kwamba Flossie alikuwa paka maalum, lakini sikufikiria ningeshiriki nyumba yangu na mmiliki wa rekodi ya ulimwengu,"

Madaktari huku wakipigwa na butwaa walisema "Tulishangaa tulipoona kwamba rekodi za daktari wa mifugo aliyekuwa anampa matibabu Flossie, zilionyesha kuwa ana umri wa miaka 27,"  na hapo ndipo habari za umri wake wa ajabu zilianza kuenea na safari ya kuingia kwenye rekodi ya dunia ilianza.