Israel ilitumia zaidi ya dola bilioni moja kuzuia mashambulizi ya Iran

Gharama hii haijumuishi hasara iliyopatikana kwenye uwanja,hasara ambayo jeshi la Israel liliitaja kuwa ni ndogo.

Muhtasari

Israel ilitumia zaidi ya dola bilioni moja kuzuia mashambulizi.Israel ilitumia zaidi ya dola bilioni moja kuzuia mashambulizi ya  mianots.

Iran ilifanya mashambulizi dhidi ya Israel, Aprili 14, 2024
Iran ilifanya mashambulizi dhidi ya Israel, Aprili 14, 2024
Image: EPA

Gazeti la Yedhith Athronoth lilimnukuu kiongozi wa zamani wa kijeshi akisema kuwa Israel ilitumia zaidi ya shekeli bilioni 5 ( sawa na dola bilioni 1.35), usiku mmoja wakati wa kukabiliana na shambulizi lililoanzishwa na Iran dhidi ya Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora.

Mshauri mkuu wa zamani wa majeshi ya Israel Ram Aminach, alisema kuwa shambulio la Iran liligharimu Israel kati ya shekeli bilioni 4 na bilioni 5 ( kati ya dola bilioni 1.08 na bilioni 1.35), na akaongeza kuwa gharama hizo zinahusu tu kukabiliana na ndege zisizokuwa na rubani na makombora kutoka Iran.

Gharama hii haijumuishi hasara iliyopatikana kwenye uwanja,hasara ambayo jeshi la Israel liliitaja kuwa ni ndogo.