Yesu wa Tongaren hana kesi ya kujibu-Mashtaka

Hii ni baada ya serikali kusema hakuna ushahidi wa kutosha wa kumshtaki.

Muhtasari
  • Aliongeza kuwa alikuwa akifahamiana vyema na Yesu wa Tongaren, ikizingatiwa kwamba walikuwa wakiishi eneo moja.
akizungumza na waandishi wa habari alipojiwasilisha mbele ya mkuu wa polisi wa Bungoma Francis Kooli mnamo Mei 10, 2023.
Yesu wa Tongaren akizungumza na waandishi wa habari alipojiwasilisha mbele ya mkuu wa polisi wa Bungoma Francis Kooli mnamo Mei 10, 2023.
Image: SCREENGRAB

Upande wa mashtaka sasa unasema Mhubiri  Eliud Wekesa almaarufu Yesu Wa Tongaren hana kesi ya kujibu.

Hii ni baada ya serikali kusema hakuna ushahidi wa kutosha wa kumshtaki.

Alikuwa ameshutumiwa kwa uendeshaji kinyume cha sheria wa jamii isiyosajiliwa, misimamo mikali na ulaghai wa fedha lakini Jumanne upande wa mashtaka ulisema hauna ushahidi.

Kiongozi wa Chama cha Roots George Wajackoyah alimwakilisha Yesu wa Tongaren mahakamani.

Wekesa alikuwa amezuiliwa na polisi kwa siku nne zilizopita alipokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kiakili, baada ya kutangazwa kuwa na matatizo ya kiakili.

"Mahakama imekubali na kutoa kibali kwa upande wa mashtaka kumzuilia mshukiwa kwa siku nne zaidi ili kuwaruhusu kukamilisha uchunguzi na kufanya tathmini ya kiakili," Olando alisema.

Wiki iliyopita, aliitwa na afisa wa DCI wa Bungoma Elijah Macharia kuhojiwa kuhusu kanisa lake la New Jerusalem na amekuwa akizuiliwa na polisi.

Haya yanajiri siku moja baada ya baadhi ya wabunge wa Bungoma kuchukua hatua na kumtetea muhubieri huyo,huku wakisema wanataka aachiliwe.

Wakiongozwa na mbunge wa Tongaren John Chikati, wabunge hao waliongeza kuwa kuachiliwa kwa mhubiri huyo hakufai kujumuisha masharti ya dhamana.

"Na tunauliza ya kwamba atolewe bila masharti yoyote. Asipatiwe bond yoyote atolewe on free bond.

Aliongeza kuwa Yesu wa Tongaren hakuwasilisha madhara yoyote, akisema alikuwa mtu aliyelenga kuombea watu.

"Anaombea Papa wa Roma akuwe rais. Yesu wa Tongaren aachiliwe."

Aliongeza kuwa alikuwa akifahamiana vyema na Yesu wa Tongaren, ikizingatiwa kwamba walikuwa wakiishi eneo moja.

Chikati aliandamana na Mbunge wa Webuye Mashariki Martin Wanyonyi.