Uhalifu haulipi

Uhalifu wamletea mwanamke ujane mapema

Dunia yake ilisimama kwa muda na akajiona ni kana kwamba alikuwa katika ndoto mbaya .

Muhtasari
  • Mwaka wa 2018 ulipokuwa ukikaribia kuisha , Cathy alijiambia kwamba mwaka mpya ufuatao wa 2019 ungekuwa mwanzo mpya kwake na mume wake
  • Kulikuwa na uvumi kuhusu kazi ya mume wake lakini  kimoyo moyo Cathy hakutaka kutoa mjadala huo  kwa sababu yeye alifiriki atambadilisha Oti aache uhalifu kisha waondoke mtaa huo na kuanza maisha kwingine kwa njia nzuri

Cathy  Kambua haamini kwamba   maisha yanaweza kuchukua mkondo mwingine kwa kasi na kukuacha hoi katikati ya usichojua .

 Maisha yake  yamekuwa kama mashindano ya langa langa ,kasi ya juu Zaidi na kisha yanafika kikomo kwa ghafla .  Ameachwa kuwa mjane mwaka mmoja tu tangu kuanza kuishi na  kijana mmoja   Oti kama mume wake . Mambo hayajakuwa rahisi  katika uhusiano wao wa miaka mitatu  hadi walipofika hatua ya kukubaliana kuanza kuishi pamoja .

 Katika mtaa wa mabanda wa korogocho ,kila  siku ni mapambano ya kufikia siku ya pili na  cha mwisho ambacho Cathy aliwahi kufikiri kitafanyika ni mume wake  Otis kupigwa risasi wakati yeye na genge jingine la wahalifu walipowekewa mtego na polisi katika eneo la Pangani walipokuwa wamekwenda kutekeleza wizi  katika kituo kimoja cha petrol . Kulikuwa na uvumi kuhusu kazi ya mume wake lakini  kimoyo moyo Cathy hakutaka kutoa mjadala huo  kwa sababu yeye alifiriki atambadilisha Oti aache uhalifu kisha waondoke mtaa huo na kuanza maisha kwingine kwa njia nzuri . Alifikiri baada ya muda kwa sababu ya mapenzi yao angeweza kumshawishi mpenzi wake  akome kuendelea na maisha yale ambayo  kila siku akirejea ilikuwa ni kama bahati kwa sababu kando na visa vya kuponea kuuawa pia kulikuwa na hatari   uhasama wa magenge ya ndani kwa ndani yaliyokuwa yakilumbana na baadhi ya vijana katika magenge hayo walikuwa na bunduki .

Mwaka wa 2018 ulipokuwa ukikaribia kuisha , Cathy alijiambia kwamba mwaka mpya ufuatao wa 2019 ungekuwa mwanzo mpya kwake na mume wake .Tayari alikuwa ashapata nyumba na  kazi katika mji  wa Emali ambako kakake alikuwa na hoteli .Kibarua kwake kilikuwa tu kumshawishi Oti akubali waondoke ili aachane na uhalifu .

 Mipango yake ilisalia kuwa ndoto kwani usiku ya tarehe 23 disemba mwaka wa 2018 zilienea ripoti kuhusu genge la vijana wadogo waliouawa na polisi kwa kupigwa risai ng’ambo ya pili . Cathy hakuhitaji kuambiwa kwamba ndio uliokuwa  mwisho wa maisha ya ndoa na Oti .Isitoshe ,yalikuwa yamemgonja mbele kwa sababu baada ya kuthibtishwa kwa habari hizo ,mtoto wa kike alizarai na alipopelekwa hospitali ,madaktari walikuwa wamemngoja na habari nyingine-Alikuwa mja mzito . Dunia yake ilisimama kwa muda na akajiona ni kana kwamba alikuwa katika ndoto mbaya .

Baada ya mwaka mmoja ,Cathy alikuwa ameachwa mjane na mimba bila lolote huku majirani nao wakimtazama kama sehemu ya genge la uhalifu ambalo lilikuwa limetambulika kwa kuwahangaisha watu .Hakuna aliyekuwa tayari kumsikiza na hivyo basi hakutarajia huruma kutoka kwa yeyote . Miaka miwili baadaye ,Cathy yungali anajutia kuhusu kujikokota kwake katika kumtoa mume wake kwenye uhalifu.Maisha nayo lazima yaendelee na mafunzo yake