Fahamu dalili zinazoashiria kuwa huenda unaugua saratani ya matiti

Wataamu wameshauri wanawake kujifikisha kwenye vituo vya afya mapema kupimwa kubainisha iwapo wanaugua ugonjwa huo kwani unaweza thibitiwa unapogunduliwa mapema.

Muhtasari

•Saratani ya matiti ni ukuaji usiodhibitika wa seli kwenye matiti unaosababisaha kinundu/uvimbe. Uvimbe wa saratani unaweza enea hadi kwenye sehemu zingine za mwili.

cancer.drugs
cancer.drugs

Saratani ni ugonjwa unaoibuka baada ya kuharibika au kubadilika kwa seli mwilini  na kuanza kuzaliana kwenye mwili.

Kuna aina nyingi za saratani zikiwemo saratani ya mapafu, matiti, damu, koo, kibofu cha mkojo, ngozi, mdomo, ovari, utumbo na nyinginezo

Aina moja ya saratani ambayo imewaathiri na kuangamiza wanawake wengi ni saratani  ya matiti.

Madaktari wamewashauri wanawake kujitokeza  mapema kupimwa kubainisha iwapo wanaugua ugonjwa huo kwani unaweza thibitiwa unapogunduliwa mapema.

Saratani ya matiti ni ukuaji usiodhibitika wa seli kwenye matiti unaosababisaha kinundu/uvimbe. Uvimbe wa saratani unaweza enea hadi kwenye sehemu zingine za mwili.

Tumeangazia baadhi ya ishara zinazoashiria kuwa huenda mwanamke anaugua saratani ya matiti. Hizi hapa ishara:

Uchungu kwenye titi ama chuchu

Uvimbe, joto au kubadilika kwa rangi ya kawaida ya titi kuwa nyekundu au nyeusi zaidi.

Kubadilika kwa saizi au umbo wa titi.

Kubonyea au kukunjika kwa ngozi.

Kuwa na mwasho, kidonda, upele au magamba kwenye chuchu

Chuchu kutokwa na  maji yasiyo ya kawaida ghafla.

Chuchu au sehemu nyingine ya titi kujikunja ndani.

Kuwa na kinundu au fundo gumu kwenye titi.

Kunenepa kwa ngozi ya titi au makwapa.

•Upele kwenye titi.

(Hisani, Wizara ya Afya nchini Kenya, MoH)

Ni vyema kutembelea kituo cha afya na kupimwa iwapo unashughudia dalili hizi mwilini. Unavyogundua mapema kuwa unaugua saratani ndivyo nafasi yako ya kupona inakuwa kubwa.