Fahamu mambo 10 ya kushangaza kuhusu pweza

Pweza wana mioyo mitatu!

Muhtasari

•Kama ni pweza dume huwa ananyoosha mkono wake kumpandia jike na kama pweza jike akikubali basi manii yatapita chini ya mkono.

Image: GETTY IMAGES

Akiwa na seli za ubongo zinazomzunguka mwili wake wote, pweza ni kiumbe machachari, mdadisi ambaye ana uwezo ambao unaweza kukushangaza.

Katika kitabu cha sauti cha mwanafalsafa na mzamia maji Peter Godfrey-Smith kinachoitwa 'Other Minds': kinaangazia maisha ya pweza katika uwezo wake wa kufikiri na mabadilko ya kushangaza ya kiumbe huyo.

Haya ni mambo machache ambayo yatakushangaza tuliojifunza kuhusu kiumbe huyu asiyekuwa na uti wa mgongo.

1. Ni viumbe wenye akili sana na ubongo wao upo kwenye mikono

Image: GETTY IMAGES

Pweza wana mfumo mkubwa wa neva na wastani wa karibu milioni 500 wa seli au seli za ubongo.

Hali ambayo inamuweka kuwa na ubongo unaofanana na mamalia wadogo kama mbwa.

Sio kama mbwa , binadamu au wengineo, neva zake ziko mikononi na sio kwenye ubongo, kwanza ni kama ziko karibu mara mbili ya wingi wa idadi yake.

Katika kila mkono wa pweza unaweza kuwa na neva 10,000 ambazo unaweza kuzishika au kuzionja.

2. Pweza anaweza akafundishwa na ana uwezo wa kukumbuka

Image: GETTY IMAGES

Utafiti wa miaka saba iliyopita unaonesha kuwa pweza anaweza kufundisha kufanya vitu vidogo vidogo .

Katika jaribio moja, pweza kadhaa waliweza kuwasukuma dagaa ili wapate tuzo.

Pweza wameweza kufanya majaribio kadhaa ya kuangalia na kukumbuka, kwa kufunga jicho moja na kuacha lingine.

Ni mchakato mrefu, lakini pweza alifanikiwa kulifanya ukitofautisha na wanyama wengine wengi.

3. Ni viumbe watukutu sana

Image: GETTY IMAGES

Katika jaribio la kuweza kuinua mzigo lililotajwa awali , pweza watatu walishiriki na kupewa majina ya Albert, Bertram na Charles. Albert na Bertram ndio walikuwa wanafuata maelekezo vizuri wakati Charles alikuwa anataka kuuvuruga tu huo mzigo.

Kama fujo hizo zilikuwa hazitoshi, Charles alikuwa akimwagia maji zoezi lolote alilopewa kufanya siku hiyo.

Pweza ambao walikuwa na fujo waliripotiwa mara kadhaa wakiwa majini, wakiwemo wale waliojifunza kuwasha na kuzima taa na kusambaza umeme kwa kutumia ndege.

Katika chuo kikuu cha Otago kilichopo New Zealand, fujo zao zilikuwa zinasababisha gharama kubwa hivyo iliwabidi kuwarudisha pweza hao majini.

4. Pweza wana uwezo wa kumtambua mtu

Image: GETTY IMAGES

Katika maabara hiyo hiyo ya New Zealand ambayo ilkuwa inafanya jaribio la taa na kushindwa, pweza walikuwa wanaweza kutambua wafanyakazi wa hapo kwa kuonesha kuwapenda baadhi na wengine kuwachukia bila ya kuwa na sababu.

Mtu anayemchukia akipita lazima amwagie maji mgongoni kwenye shingo.

5. Pweza wanapenda kucheza

Image: GETTY IMAGES

Pweza ni viumbe wanaopenda kucheza.

Baadhi ya pweza waliokuwa katika maabara walionekana wakitumia muda mwingi kwa kurushiana makopo ya vidonge, kupiga kelele kwenye maji na kurukaruka kwenye maji.

6.Pweza wanazaliana kwenye mikono

Image: GETTY IMAGES

Katika viumbe wengi kama pweza, huwezi kugundua kama ni jike au dume kama wakiwa wamejikunyata katika mikono yao.

Kama ni pweza dume huwa ananyoosha mkono wake kumpandia jike na kama pweza jike akikubali basi manii yatapita chini ya mkono.

Mara nyingi jike huwa anahifanyi manii kwa muda kabla ya kuanza kurutubisha mayai yao.

7. Wana namna yao ya kusalimia

Image: GETTY IMAGES

Wakati pweza wanapokuwa wanatembea mara nyingine huonekana "wakitoa wenzao kwenye maficho wakitumia mikono.

Hata hivyo , Profesa Stefan Linquist, ambaye amesomea tabia ya pweza, anaamini kuwa huwa wanasalimiana kwa mkono na tabia hiyo inawasaidia pweza kutambuana.

8. Pweza wana mioyo mingi

Image: GETTY IMAGES

Pweza wana mioyo mitatu!

Mioyo yao inasukuma damu ambayo ina kijani na blu

Wanatumia shaba kama oksijeni yao badala ya chuma ambayo inatufanya tuwe na damu nyekundu.

9. Wanaweza kukutisha sana

Image: GETTY IMAGES

Pweza ana uwezo wa kubadilisha rangi na muundo wake.

Wakati dume mwenye hasira akiwa akitaka kumshambulia pweza mwingine, mara nyingi atageuka kuwa mweusi, atainuka kutoka kwenye bahari, na kunyoosha mikono yake kwa njia ambayo inakuza umbo lake.

Wakati mwingine atainua vazi lake, sehemu yote ya nyuma ya mwili wake, juu ya kichwa chake - hii inaitwa jina la "Nosferatu" na kuwa na muonekano wa kutisha.

10. Na ana faida ya kutokuwa na mifupa

Image: GETTY IMAGES

Pweza anaweza kujibana kwenye shimo karibu na umbo la mboni yake na kubadilisha sura ya mwili wake.

Kutokuwa na mifupa au ganda sio kawaida kwa mnyama aliye na umbo na uwezo kama wa pweza.

Sifa hii inawafanya wawe katika hatari zaidi kwa wanyama wanaokula wenzao kwa kiwango kimoja, lakini pia huwawezesha kujificha.