Fahamu majibu kuhusu umri wa mwanamke unavyoathiri maisha ya ndoa

Ukomo wa hedhi si ugonjwa, ni mabadiliko ya kawaida yanayomfikia mwanamke.

Muhtasari

•Mwanamke anaingia kwenye hatua hii ya kukoma kwa hedhi akiwa na nguvu zake na si lazima awe mzee.

•Wanawake ambao wamefikia ukomo wa hedhi wanakuwa na matatizo ya kuumwa kichwa na viungo vingi vya mwili na pia kuhisi kulemewa mambo.

•Kutokana na mabadiliko mengi yanayojitokeza wakati wa kukoma kwa hedhi kama kuwa wakavu,kupoteza hamu, mabadiliko ya ngozi, Dr. Yelwa anasema kuwa kuna tiba ambazo mwanamke anaweza kupata au kutumia

Image: GETTY IMAGES

Katika kila hatua , kuna mabadiliko ya kibaiolojia kama ya kupata hedhi, kujifungua na kulea.

Mabadiliko mengine katika maisha ya mwanamke, ni kukoma kwa hedhi na ukomo wa kupata watoto ambako kunajulikana kama Menopause.

Kukoma kwa hedhi ya 'Menopause'kuna maana gani?

Dkt Yelwa, mtaalamu wa mausala wa kukoma kwa hedhi katika hospitali ya Maitama mjini Abuja, anasema hatua hii ya Menopause huwa ni wakati ambao mwanamke anakosa hedhi.

Mwanamke anaingia katika hatua hii kama hajaweza kupata siku zake za hedhi kwa kipindi cha miezi 12.

Mwanamke anakuwa mtu wa kawaida tu pale ambapo kiwango cha mamilioni ya seli katika mwili wake zinapungua na kufanya utamaduni ambao ulikuwa umezoeleka kwa miongo kumaliza muda wake.

Ukomo wa hedhi si ugonjwa, ni mabadiliko ya kawaida yanayomfikia mwanamke.

Mwanamke anaingia kwenye hatua hii ya kukoma kwa hedhi akiwa na nguvu zake na si lazima awe mzee.

"Mwanamke anakuwa hana hamu ya wanaume sana kutokana na kupungua kwa homoni ambazo zinasaidia damu zinazoitwa 'estrogen'"kwa mujibu wa daktari.

Kuna dalili nyingi ambazo mwanamke anaweza kuzihisi wakati anataka kuingia katika hatua hiyo ya ukomo wa hedhi.

Wanawake wanapitia hatua mbalimbali katika maisha yao, tangu wanapozaliwa, wanapovunja ungo na kuingia hatua ya utu uzima.

Image: Dr Yalwa Usman

Kwa kawaida mwanamke anafikia ukomo wa hedhi akiwa na miaka 45 mpaka 55.

Lakini daktari anasema watu wengi huwa wanaacha kupata hedhi katika umri wa miaka 51.

"Mwanamke anaweza kukoma kupata hedhi kwa muda kama imba ilitoka, alijifungua kabla ya muda au alijifungua kwa njia ya upasuaji."

Dkt. Yalwa anasema matatizo yote haya yanaweza kutokea kwa mwanamke muda wowote ule.

"Mwanamke anaweza kupata matatizo ya hedhi si kwasababu ni mzee."

Hata hivyo daktari anasema baadhi ya wanawake bado wanapata hedhi hatakama wana umri wa miaka 60 ingawa kwa kawaida wanapaswa kuwa wameacha kupata hedhi katika umri wa miaka 45 mpaka 55.

Dalili zake

Kwa kawaida hatua huwa zinapishana na mabadiliki hayaji kwa mara moja.

Daktari anasema wanawake wanaweza kugundua baadhi ya mabadiliko mapya na ishara za kuingia katika hedhi.

"Mabadiliko hayo yanajumuisha mzunguko wa hedhi , kwa mfano,kama mwanamke amepata siku zake za hedhi kila baada ya siku 30 au 28 na mara ataanza kuona siku zake anazipata baada ya siku 40,au hata miezi miwili inapita bila kupata siku zake za hedhi."

Hivyo mwanamke anaweza kuanza kuona mabadiliko katika kiwango cha hedhi anayopata ikiwa tofauti na ile ya awali.

Daktari anasema kuwa kama mwanamke alikuwa anapata kwa siku tano au saba , anaweza kurudi kupata kwa siku mbili.

Na wengine kuwa zaidi ya siku saba.

Dalili nyingine kwa wanawake kufikia ukomo wa kupata hedhi , unajumuisha kutokwa na jasho sana hata kama ni wakati wa baridi.

Vilevile mwanamke anaweza kutumia muda mwingi kabla hajalala usiku au akiamka usiku inakuwa shida kwake kupata usingizi tena.

Wanawake ambao wamefikia ukomo wa hedhi wanakuwa na matatizo ya kuumwa kichwa na viungo vingi vya mwili na pia kuhisi kulemewa mambo.

Ishara nyingine za kukoma kwa hedhi , wanawake wanapoteza nywele, ngozi zao kuwa kavu na mwanamke anahisi kutotaka kufanya ngono na mume wake.

"Kama akifikia hatua hii , ataanza kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana badala ya kujihisi vizuri."

Daktari alisema wanawake wanaweza kuhisi mabadiliko wa mpango wa uzazi , wakati wa kujifungua na kupoteza hamu ya kujamiiana, "Dkt. Yelwa anasema.

Anaongeza kusema kuwa hizi zote ni zinatokea wakati ambao homoni za mwanamke za 'estrogen' zikiwa chini sana.

Je inawezekana kwa damu kurudi baaada muda wa ukomo wa hedhi?

Daktari anasema kuwa baada ya kipindi cha kupata hedhi kukoma, anaweza akapata hedhi tena baada ya miezi 10 hivi au mwaka.

'Mara nyingine mwanamke anapata hedhi baada ya kukutana na mume wake wakati akiwa hatua ya ' menopause '.

Lakini daktari anasema kuwa hilo si jambo zuri, inabidi mwanamke aende hospitali haraka iwezekanavyo kwa ajili ya vipimo vya afya.

Image: GETTY IMAGES

Mwanamke anapaswa kufanya nini kabla ya muda wa kukoma hedhi ?

Daktari alisema hatua ya kwanza ni mwanamke kuelewa hali yake ya afya , na kuelewa tatizo na kiwango cha kukoma kwa hedhi.

Ni muhimu kwa mwanamke kuelewa tatizo ambalo atakutana nalo kabla ya kuingia hatua hiyo ambayo itakuwa na mabadiliko makubwa katika mwili wake.

Daktari anasema hospitali wanaweza kukusaidia kuweza kutofautisha kati ya ugonjwa na dalili za ukomo wa hedhi.

Kama mtu anatokwa na damu kwa wingi akiwa anaharisha, basi kuna tatizo inabidi uende hospitalini kwa ajili ya vipimo.'

Baadhi ya wanawake wanalalamika kuwa wanasumbuliwa na kukoma kwa hedhi hata kabla hawajafika miaka 30.

Matatizo kama ya kuwa mkavu katika sehemu za siri na kukosa hamu ya kujamiiani ambayo yanaweza kupelekea katika matatizo kati ya wanawake na waume zao.

Je mwanamke anaweza kupata tiba ili kupunguza muda wa kufikia kikomo cha hedhi?

Kutokana na mabadiliko mengi yanayojitokeza wakati wa kukoma kwa hedhi kama kuwa wakavu,kupoteza hamu, mabadiliko ya ngozi, Dr. Yelwa anasema kuwa kuna tiba ambazo mwanamke anaweza kupata au kutumia.

Lakini pale tu daktari anapotoa ushauri kuwa tiba flani itumike kwa kuwa ni matibabu sahihi.

Kwa mujibu wa daktari , bara la ulaya kuna ambao wanapata tiba ya ya homoni au matumizi ya dawa za asili pia na mazoezi.