Fahamu majukumu ya Meneja wa wanamuziki katika tasnia ya uimbaji

Baadhi ya maneja wa wasanii nchini Kenya ni kama Kash Keed, Kaka Empire inayomilikiwa na msanii King Kaka, Dreamland Music Empire na zingine.

Muhtasari

• Hivi majuzi msanii Otile Brown alitangaza uamuzi wa kutengana na meneja wake wa miaka sita, Joseph Noriega.

• Wasimamizi  hawa pia huwapangia matamasha, maonyesho ya matangazo na mahojiano na vyombo vya habari.

Studio ya kurekodi muziki
Studio ya kurekodi muziki
Image: STAR

Baada ya Mwalimu Rachel kujitokeza na kusema kuwa anajutia kujihusisha na waimbaji wa Genge Tone, Sailors. Niliamua kuweza kufahamu kwa ndani jukumu la meneja kwa maisha na kazi ya wasanii.

Hivi majuzi msanii Otile Brown alitangaza uamuzi wa kutengana na meneja wake wa miaka sita, Joseph Noriega.

Baadhi ya meneja wa wasanii nchini Kenya ni kama Kash Keed, Kaka Empire inayomilikiwa na msanii King Kaka, Dreamland Music Empire na zingine.

Lakini ni ipi kazi ya meneja hawa hasa? Wanahusika vipi na maisha ya kibinafsi ya wasanii wanao wawakilisha? Wanahusika vipi na pesa za wasanii wanaosimamia?

Jukumu kuu la meneja hawa wa wasanii ni kuwawakilisha wateja wao katika shughuli na mazungumzo za kibiashara na pia kukuza taaluma za wateja wao.

Kazi ya wasimamizi hawa wa muziki sio tu kuwasaidia wasanii kupanga taaluma zao na kuangazia malengo yao ya muda mrefu ya kikazi, lakini pia husaidia kushughulikia kazi za kila siku za wasanii wao.

Meneja hawa huwashauri wateja wao kuhusiana na wimbo bora kufanya na jinsi ya kuifanya, ni nani wanaweza shirikiana nao kimziki, ni studio gani wanaweza kuenda ili wimbo wao uweze kuenea vikubwa.

Watu hawa muhimu katika taaluma ya wasanii huhusika pakubwa kujadili mikataba ya kibiashara na pia kukusanya malipo kwa niaba ya wateja wao.

Wasimamizi  hawa pia huwapangia tamasha, maonyesho ya matangazo na mahojiano na vyombo vya habari.

Ikiwa meneja huyo anaiwakilisha bendi na kuweze kuibuka migogoro ya kibinafsi baina ya wanachama wa bendi hiyo basi meneja huyo ana jukumu la kusuluhisha tatizo hilo.

Mahausiano ya meneja na msanii anayemsimamia inaweza kukua na kufikia pahali ambapo meneja huamua ni nani mteja wake anaweza kuwa na mahusiano ya kirafiki naye, ni wapi ataenda na ni saa ngapi ataenda na kufanya shughuli zake.

Kuna hatari ya meneja hawa kumshauri ata mteja wake kuhusu mahusiano ya kimapenzi na pia kuathiri uamuzi wa muimbaji katika mahusiano hayo.

Kwa hakika kazi ya meneja hawa huwa kwa mara mingi haitambuliki lakini hawa ndio huwa na uwezo waikufanya taaluma ya msanii kuimarika ama kuende sege mnege.