Otile Brown atengana na meneja wake baada ya miaka sita

Wawili hawa wametengana baada ya kufanya kazi pamoja kwa miaka saba sasa.

Muhtasari

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Instagram siku ya Jumanne, Otile aliangaza habari za kutengana kwao.

Otile aliwahakikishia mashabiki wake kwamba licha ya kuachana na Noriega, ataendelea kufanya muziki wake.

Otile Brown na Meneja wake Joseph Noriega.
Otile Brown na Meneja wake Joseph Noriega.
Image: INSAGRAM

Mwanamziki Jackob Obunga almaarufu Otile Brown wametengana na meneja wake Joseph Noriega baada kufanya kazi pamoja kuanzia mwaka wa 2017 na kupata mafanikio mengi kimziki.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Instagram siku ya Jumanne, Otile alitangaza habari za kutengana kwao, akitaja wakati wao pamoja kama "Safari ya Ajabu".

Otile alitoa shukrani kwa Noriega kwa jukumu lake kubwa la kumtengeneza kama msanii katika safari yake yote ya muziki.

"@noriega_donself barikiwa mfalme, nakupenda daima. Asante kwa safari, kumbukumbu zote na mafanikio tuliyoyapaa aia safari hii ya muziki . Nimefurahishwa na kile kitakachotokea mbeleni, "Brown aliandika.

Noriega kwa upande wake alimshukuru Otile Brown kwa kumbukumbu na mafanikio  waliopata pamoja.

“Nashukuru kwa safari, Kumbukumbu na mafanikio yetu pamoja…..Mungu akubariki,” Noriega alisema.

Otile aliwahakikishia mashabiki wake kwamba licha ya kuachana na Noriega, ataendelea kufanya muziki wake.

"Ingawa Noriega atakosekana, Otile Brown anaendelea kujitolea kwa safari yake ya muziki kwa ari na ari sawa. Mashabiki wanaweza kuwa na uhakika kwamba maono ya Brown na muziki wa kipekee utaendelea,” ilisoma taarifa kutoka kwa lebo ya mwimbaji huyo, Just In Love Music.