(+Video) Kanisa lamfukuza kazi Padre aliyeonekana akibusu wanafunzi

Video ilimuonyesha kiongozi wa dini aliyevaa nguo za kijani akiwaita wanafunzi watatu wa kike kwenye mimbari, na kisha akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu, huku kelele za kushangiliwa zikisikika.

Muhtasari

•Kanisa limemfukuza padre Balthazar Obeng Larbi siku ya Jumannne baada ya kukaa kikao na kujadili suala hilo.

Image: HISANI

Kanisa la Anglikana nchini Ghana limemfukuza kazi padre aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mtandaoni, akiwabusu wanafunzi.

Kanisa limemfukuza padre Balthazar Obeng Larbi siku ya Jumannne baada ya kukaa kikao na kujadili suala hilo.

Wakati uchunguzi ukiendelea, kanisa limekuja na maamuzi ya kumfukuza padre huyo wa chuo cha Mt. Monica.

Kufukuzwa kwa padre huyo kutawadhihirishia umma hatua waliyoichukua, pamoja na kuwapa ushauri nasaha mabinti watatu walioonekana kwenye video.

Padre Balthazar Obeng Larbi amezuiwa kufanya shughuli zote za utumishi wakati uchunguzi ukiwa unaendelea na kufuata ushauri kutoka kwa kamati iliyoundwa kwa ajili kushughulia suala la padre huyo.

Katika taarifa ya kanisa hilo, imeelezea kusikitishwa na tukio hilo na uchunguzi umeanza mapema.

Taarifa hiyo imeeleza wanafunzi hao watatu watapewa ushauri nasaha ili kuondoa mshtuko waliopata.

Katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha kiongozi wa dini aliyevaa nguo za kijani akiwaita wanafunzi watatu wa kike kwenye mimbari, na kisha akawavua barakoa zao kabla ya kuwabusu, huku kelele za kushangiliwa zikisikika.

"Nimechukizwa sana na hata sielewi. Inawezekanaje hili kutokea kwenye Taasisi ya elimu?," mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter aliandika. Mwingine akaandika: "Baba mchungaji anawabusu wanafunzi watatu mbele ya shule nzima. Aibu!"