Vijana watatu wanaodaiwa kuuzia makahaba dawa za kulevya wakamatwa Mwingi

Muhtasari

•John Musya, Paul Mumo na Julius Musya walikamatwa  wakiuza aina tofauti ya madawa ya kulevya ikiwemo heroin baada ya masaa ya kafyu usiku wa Jumapili.

Pingu
Image: Radio Jambo

Washukiwa watatu wa ulanguzi wa dawa za kulevya wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamatwa wakiendeleza biashara yao katika mji wa Mwingi.

John Musya, Paul Mumo na Julius Musya walikamatwa  wakiuza aina tofauti ya madawa ya kulevya ikiwemo heroin baada ya masaa ya kafyu usiku wa Jumapili.

Inadaiwa kuwa watatu hao wamekuwa wakiuzia makahaba mihadarati hiyo wakati wanaendeleza biashara yao ya usiku

Kulingana na DCI, zaidi ya misokoto 10 ya bangi pia ilipatakina mikononi mwa washukiwa.

Watatu hao watashtakiwa kwa kosa la kupatikana na dawa  za kulevya pamoja na kuendeleza biashara hiyo.