Urusi inaomba uungwaji mkono wa nchi za Afrika

Nchi nyingi katika bara la Afrika haziko tayari kuegemea upande wowote katika vita vya Ukraine.

Muhtasari

• Kwa sasa, kuongezeka kwa bei za chakula na mafuta ni jambo linalotia hofu kubwa barani Afrika.

• Asilimia 40 ya nchi za Afrika kila mwaka huagizwa bidhaa za vyakula kutoka Ukraine na Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov
Image: BBC//EPA

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov anajaribu kuyashawishi mataifa ya Afrika  kwamba walipaswa kuwa upande wa Urusi badala ya nchi za Magharibi. Kwa sababu hii, anatumia maelezo kama, "tutawasaidia katika mchakato wa kumaliza ukoloni " katika mikutano yake rasmi.

 Hatahivyo, nchi nyingi  katika bara hilo haziko tayari kuegemea  upande wowote katika vita vya Ukraine. Kwasababu zainakumbuka vyema athari za vita baridi vya dunia  kwa Afrika, ambavyo vilisababisha mizozo na kurudisha nyuma maendeleo. 

 Kwa sasa, kuongezeka kwa bei za chakula na mafuta ni jambo linalotia hofu kubwa. Asilimia 40 ya nchi za Afrika kila mwaka huagizwa kutoka Ukraine na Urusi.

 Viongozi wa Afrika pia wanafahamu fika kwamba kadri uhaba wa chakula unaendelea kuwa mbaya zaidi, wanakabiliwa na uwezekano wa kutoendelea kubakia mamlakani.

Wakati wa wa ziara yake nchini Misri, Waziri wamambo ya nje wa Urusi  Sergey Lavrovalikana madai kwamba Urusi ndio inayosababisha mzozo wa chakula.   

 Akizungumza mbele ya wanadiplomasia  wa mataifa ya Muungano wa Kiarabu nchini Misri, Lavrov alisema kuwa mataifa ya Magharibi yanajaribu kuficha ukweli kuhusu athari za vikwazo kwa usalama wa chakula duniani.

 Lavrov aliyashutumu mataifa ya Magharibi kwa kujaribu kuyatawala mataifa mengine. 

 Lavrov alisema kwamba kuna sababu ya "uchokozi " wa mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi : " Suala sio Ukraine, suala ni hali ya baadaye ya dunia ."

 "Wanasema kwamba kila mmoja anapaswa kuunga mkono sheria. Hatahivyo, sheria hizo zimeandikwa kwa kuzingatia maslahi fulani ya nchi za Magharibi."

 Maafisa wa Urusi walisema kuwa anashukuru kwa  "msimamo usioegamia upande wowote  " ulioonyeshwa na nchi za Afrika katika vita vya Ukraine. 

 Ili kupata uungaji mkono wa Urusi, Lavrov anatarajiwa kufanya ziara katika mataifa ya  Ethiopia, Uganda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya Misri.

Misri ni nchi ya   kwanza kwanza duniani kwa uagizaji wa nafaka na mwaka jana ilinunua 80% ya nafaka zake kutoka Urusi na Ukraine.

Uvamizi wa Urusi katika Ukraine Februari, 24 ulivuruga usafirishaji wa meli wa nafaka na kusababisha mfumuko wa bei, na kusababisha  mzozo wa kiuchumi kwa Misri.

 Katika kukabiliana na athari za vita, Misri imejipata njia panda baina ya kuendelea kushikilia msimamo wake wa muda mrefu na Urusi na marafiki zake wa karibu- mataifa yenye nguvu ya Magharibi  ambayo yameiwekea vikwazo na wanataka kuitenga serikali ya Moscow. 

Balozi za magharibi zilikuwa zimetaka ushawishi kwa Misri na Mungano wa nchi za Kiarabu kabla ya ziara ya  Lavrov, ambayo ilijumuisha mazungumzo na Rais Abdel Fattah al-Sisi  na wawakilishi wa Nchi za Kiarabu. 

"Tunawahakikishia tena haja yetu ya utashi wa wauzaji wa nafaka wa Urusi kutekeleza ahadi zao," Lavrov alisema katika mkutano wa waandishi wa habari na mwenyeji wake wa Misri Sameh Shoukry.