Mbunge wa kwanza wa kike Kenya,Mama Grace aaga dunia

Mama Grace alifariki akiwa na miaka 99.

Muhtasari

•Mama Grace alikuwa mbunge na Meya wa kwanza mwanamke nchini Kenya.

 

  Aliyekuwa meya wa kwanza mwanamke wa Kenya, kuchaguliwa,Mama Grace ameaga dunia.Alichguliwa mjini Kisumu mwaka wa 1965. Grace alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge, wa Mji wa Kisumu mwaka wa 1969 na kuhudumu hadi 1983. Pia alikuwa mwanamke wa kwanza katibu mkuu wa Muungano wa Wajaluo (Afrika Mashariki) na diwani wa kwanza mwanamke wa wadi ya Kaloleni huko Kisumu.

 Mama Grace alifariki akiwa na umri wa miaka 99. Alifariki katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga siku ya Jumatano. Alikuwa mgonjwa.

 

Ameombolezwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba ninakubali kufariki kwa mama Grace Onyango katika siku ambayo dunia nzima tunasherehekea mafanikio ya wanawake kipekee," alisema. "Nyabungu kama tulivyomwita kwa furaha aliangazia mazingira huru ya kisiasa ya Kenya kwa hatua ya 'wa kwanza'. Ilikuwa kawaida kutarajia 'mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kitu' kila mara jina lake lilipotajwa. Alikuwa kiongozi na mvumbuzi wa kilele. "

Pia alimtaja kama mzungumzaji asiye na woga wa masuala ya kitaifa na mtetezi mahiri wa mizizi yake. Raila alisema yeye pia alikuwa sauti ya pekee ya wananchi wakati ambapo ilikuwa hatari kusimama na kuhesabiwa.

 

Mwalimu huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa pia alikuwa mwanamke wa kwanza kamishna msaidizi wa Chama cha Girl Guides na mwenyekiti wa Jumuiya ya Ustawi wa Watoto, wilayani Kisumu.