Gabriel Oguda na wanaharakati maarufu wa mitandao wanaodaiwa kutekwa nyara

Osama Otero pia ni miongoni mwa waliotekwa nyara

Muhtasari

• Miongoni mwa waliochukuliwa ni pamoja na mwanaharakati wa kisiasa Gabriel Oguda.

•Alikuwa miongoni mwa angalau watu kumi ambao walikusanywa Jumanne, Juni 25, ripoti ziliarifu.

Gabriel Oguda
Image: Hisani

Watumiaji kadhaa wa mitandao ya kijamii na wabunifu wa maudhui hawajulikani walipo baada ya kutekwa nyara usiku wa kuamkia Jumanne 25 kabla ya maandamano ya kupinga mswada wa fedha.

Maafisa walisema hii ni miongoni mwa mikakati inayotumiwa kutuliza maandamano ya kupinga ushuru uliopendekezwa. Miongoni mwa waliochukuliwa ni pamoja na mwanaharakati wa kisiasa Gabriel Oguda.

Alikuwa miongoni mwa angalau watu kumi ambao walikusanywa Jumanne, Juni 25, maafisa walisema.

"Ninaweza kuthibitisha kuwa kaka yangu amechukuliwa na watu wasiojulikana kutoka nyumbani kwake dakika 5 zilizopita," Zachary Oguda, kakake Gabriel, 'alitweet' saa 2:53 asubuhi Jumanne.

Osama Otero ambaye amekuwa mstari wa mbele  kwenye mtandao wa X kuhusu kupinga mswada wa fedha wa 2024, pia aliripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana.

Watumiaji wengine wa X ambao wanashukiwa kutekwa nyara ni pamoja na Drey Mwangi, TemperCR7, Harriet, Shad, Franje, Worldsmith na Hilla254. Wengine wengi hawajulikani walipo baada ya kutekwa nyara na maafisa wa serikali huku kukiwa na ghasia kutoka kwa familia na marafiki.

Katika kile kilichoonekana kuwa mazungumzo yaliyoratibiwa, Osama Otero, alitweet kuhusu watu wasiowafahamu nyumbani kwake karibu wakati sawa na Oguda.

"Kuna watu nje hapa  nilipo," chapisho lake la mwisho ambalo limeenea kwa kasi ilisoma. Aidha Polisi hawajazungumza rasmi kuhusu suala hilo