Mwenyekiti wa tume ya AU ampongeza Odinga kwa kukubali uamuzi wa mahakama

Faki pia alimpongeza rais Ruto kwa kuidhinishwa kama rais wa tano na mahakama ya upeo.

Muhtasari

• Faki pia alimpongeza rais Ruto kwa kuidhinishwa kama rais wa tano na mahakama ya upeo.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga apongezwa na mwenyekiti wa tume ya AU Moussa Faki kwa kukubali uamuzi wa mahakama ya upeo
Kiongozi wa ODM Raila Odinga apongezwa na mwenyekiti wa tume ya AU Moussa Faki kwa kukubali uamuzi wa mahakama ya upeo
Image: TWITTER

Mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika Moussa Faki amempongeza kinara wa Azimio la Umoja One Raila Odinga kwa kuonesha muongozo mzuri wa kukubali uamuzi wa mahakama ya upeo.

Kiongozi huyo pia alimpongeza rais mteule William Ruto kwa ushindi wake kuidhinishwa na jopo la majaji saba wa mahakama hiyo ya upeo, ambapo rais wa idara ya mahakama Martha Koome alisoma uamuzi wao kuwa waliikiana kwa pamoja pasi na hata mmoja kupinga.

“Pongezi zangu nyingi kwa Rais Mteule Dk William Ruto baada ya kutangazwa kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya baada ya kuthibitishwa kwa matokeo ya uchaguzi,” Moussa Faki aliandika kweney ukurasa wake wa Twitter.

Faki ameungana na makumi na viongozi wengine kote ulimwenguni wanaozidi kumiminia pongezi zao kwa ushindi wa Ruto huku pia wakifurahishwa na hatua ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga kukubali matokeo, japo shingo upande.

“Napenda pia kutoa pongezi kwa uongozi wa Mhe Raila Odinga kwa kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu,” Fati alimsifia Raila.

Jana, mahakama ya upeo iitupilia mbali kesi iliyowasilishwa na muungano wa Azimio la Umoja One Kenya pamoja na wandani wake waliotaka kubatilishwa kwa matokeo ya IEBC yaliyompa Ruto ushindi mnamo Agosti 15.

Katik uamuzi wake, mahakama hiyo ilisema kwamba Ushahidi wa upande wa malalamishi haukuwa na uzito wa kufanya kesi hiyo ushindi huo kubatilishwa na hata kutaja baadhi ya Ushahidi kama uvumi usiokuwa na mashiko.