Walimshawishi baba yangu anifukuze kazi-Mwanawe Museveni adai

Bado nampenda kaka yangu mkubwa, Uhuru Kenyatta, na nina uhakika zaidi kwamba Mwenyezi Mungu yuko upande wangu

Muhtasari
  •  Muhoozi hata hivyo alijiamini bila kujali kufukuzwa kazi, akieleza kuwa aliamini kabisa kuwa Mwenyezi Mungu yuko upande wake
KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba amevunja kimya na kutuma ujumbe kwa aliyekuwa Mkuu wa Taifa wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba amemjulisha Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta kwamba anampenda sana na anamchukulia kama kaka yake mkubwa.

Jenerali Muhoozi Kainerugaba alizidi na kudai kuwa kuna kundi la watu ambao walimshawishi babake Yoweri Museveni kumfukuza kazi yake ya zamani.

Hata hivyo, Jenerali Muhoozi  hakuwafichua  watu wanaodaiwa kumshawishi babake kumfukuza kazi.

 Muhoozi hata hivyo alijiamini bila kujali kufukuzwa kazi, akieleza kuwa aliamini kabisa kuwa Mwenyezi Mungu yuko upande wake.

"Baadhi ya watu walimshawishi baba yangu anifukuze kazi yangu ya awali. Bado nampenda kaka yangu mkubwa, Uhuru Kenyatta, na nina uhakika zaidi kwamba Mwenyezi Mungu yuko upande wangu," Muhoozi Kainerugaba alisema.