Meru: Jamaa akamatwa kwa kumfungia mvulana wa miaka 16 kwa siku 3 akimlawiti

Chifu alipovamia nyumba hiyo, walimpata mshukiwa mwenye umri wa miaka 28 akitokwa na jasho huku kijana huyo mdogo akiwa uchi.

Muhtasari

• Mvulana huyo alikwenda kwa mshukiwa kutafuta msaada wa chakula kutokana na njaa.

• Alipofika, alimuahidi kuwa chakula kipo lakini alipoingia kwa nyumba alimtolea panga na kumtaka kuvua nguo zote.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mwanamume mwenye umri wa miaka 28 yuko rumande kwa madai ya kuwalawiti wavulana katika mji wa Mikinduri, Kaunti ya Meru.

Kulingana na Citizen, Mshukiwa, James Baariu Rungai, anadaiwa kunaswa huku akimlawiti mvulana wa miaka 16 ambaye inasemekana alimtishia na kumfungia ndani ya nyumba yake kwa siku tatu bila chakula.

Chifu wa eneo la Anjuki Jacob Michuki Mutiga, ambaye alifika kumsaidia mvulana huyo akiwa na wanachama wa Nyumba Kumi, alikiambia chombo hicho kwamba mshukiwa alikuwa akimlawiti kijana huyo na kumfungia ndani ya nyumba kutoka nje kwa kufuli bila chakula na maji.

Bw. Mutiga alieleza kuwa siku iliyotajwa ya uokoaji, walipokuwa wakipokea taarifa kutoka kwa umma, walivamia nyumba ya mshukiwa na kuvunja mlango.

Alibainisha kuwa, walipoingia ndani ya nyumba hiyo, walimkuta mwanaume huyo akitokwa na jasho huku kijana huyo akiwa uchi.

Msimamizi huyo aliongeza kuwa mvulana huyo aliwaambia polisi kwamba mshukiwa alimshawishi kwamba angempa chakula kwa vile anaishi na mamake katika vitongoji duni vya Mikinduri na kwa kawaida hulala njaa.

Mtoto huyo alikariri kuwa baada ya kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, alifunga mlango kwa kufuli, akaokota panga na kumwamuru avue nguo huku akitishia kumkata vipande vipande na kuutupa mwili wake chooni endapo angethubutu kupiga kelele.

Maafisa wa polisi wa Mikinduri wamewataka waathiriwa wote pamoja na wazazi wao kurekodi taarifa zao katika afisi ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ili mshukiwa afunguliwe mashtaka kulingana na uhalifu wake katika mahakama ya sheria.