Mwanamke kortini akitaka ruhusa ya kutafuta 'mpango wa kando', adai mumewe hamtoshelezi

Mrembo huyo alifumaniwa na mamake kwenye mahakama ya kusajili ndoa akiwa na mume wa pili mtarajiwa akitaka kusajili uhusiano wao huku mume wa kwanza akiwa nyumbani hajui chochote.

Muhtasari

Mama huyo alisema alipata taarifa kutoka kwa majirani zake, kwamba binti yake ameondoka kwenye nyumba yake ya ndoa.

• Mumewe kwa Mahojiano ya simu kwamba yeye na mkewe PHNET walikuwa na mtoto wa miaka 4 ambaye alimuacha nyumbani.

Mwanamke aelekea mahakamani akitaka kuruhusiwa kutafuta mpango wa kando.
Mwanamke aelekea mahakamani akitaka kuruhusiwa kutafuta mpango wa kando.
Image: Zambian Portal//Screengrab

Kizaazaa kilishuhudiwa katika mahakama moja nchini Zambia katika mji mkuu wa Lusaka baada ya mwanamke mmoja kuelekea mahakamani akitaka kibali cha kutafuta mwanamume wa kuweza kumtosheleza hitaji lake la kimapenzi – mpango wa kando – katika kile alisema kuwa mume wake hammiliki kitandani hadi mwisho wa mchezo.

Kwa mujibu wa taarifa moja iliyochapishwa kwenye mtandao wa Zambian Portal kwa njia ya video, Phinet Nkhoma, alikutwa amevaa nguo nyeupe ya harusi na ameketi karibu na mumewe mtarajiwa kwenye mahakama ya kusuluhisha maswala ya ndoa.

Aliyemfumania hapo ni Mama yake, ALICE NKHOMA katika ofisi ya Msajili wa Ndoa.

Mama huyo alisema alipata taarifa kutoka kwa majirani zake, kwamba binti yake ameondoka kwenye nyumba yake ya ndoa, akisema kuwa mumewe wa kwanza hakuwa anamridhisha kimapenzi.

Wakati huohuo, mume wa mwanamke huyo MICAH TEMBO alifichua kwa msajili wa ndoa kwamba mkewe aliondoka kwenye nyumba yao ya ndoa siku ya Ijumaa Juni 9, 2023 akidai kwamba alikuwa akienda kwa rafiki kwa ajili ya karamu na kisha angeendelea na kazi.

Bwana TEMBO aliendelea kumwambia msajili wa ndoa katika Mahojiano ya simu kwamba yeye na mkewe PHNET walikuwa na mtoto wa miaka 4 ambaye alimuacha nyumbani.

Naye Msajili wa Ndoa wa Baraza, KENNETH KANDANDU tangu wakati huo amezingatia kuwa ndoa hiyo ni batili kwani mwanamke huyo hawezi kutafuta mume mwingine kama bado ndoa na mume wa kwanza ingalipo.