Kutana na mwanamke aliyekufa na kufufuka mara 3 akibeba 'mimba' zaidi ya miaka 2

Francoise si mtu ambaye anafaa kuwa hai kwani alitajwa kuwa amefariki mara tatu na katika miaka miwili, alikuwa amebeba kile kilitajwa kuwa ni mimba.

Muhtasari

• Kwa mujibu wa simulizi hiyo ya haraka, Francoise alikuwa amepoteza matumaini ya kupata msaada wa matibabu ya ugonjwa wa ajabu.

Mama aliyebeba ujauzito wa miaka 2
Mama aliyebeba ujauzito wa miaka 2
Image: Screengrab

Simulizi ya mwanamke mmoja kwa jina Francoise aliyetajwa kufariki na kufufuka mara tatu kwa njia tatanishi imewaacha wengi na maswali mengi kuliko majibu.

Kwa mujibu wa simulizi hiyo fupi iliyopakiwa kwenye mtandao wa YouTube wa Afrimax English, Francoise si mtu ambaye anafaa kuwa hai kwani alitajwa kuwa amefariki mara tatu na katika miaka miwili, alikuwa amebeba kile kilitajwa kuwa ni mimba.

Hali yake ilibadilika katika kipindi cha miaka miwili tu na kumfyonza kila kitu alichokuwa anakimiliki, kwa kuuza ili kupata matibabu ya ‘mimba’ yake ya ajabu.

Francoise alikuwa ameolewa na pamoja na mumewe walishiriki tendo la ndoa na baadae tumbo lake likaanza kufura, kwa furaha ya mama, akadhani amepata ujauzito.

Lakini haukuwa ujauzito.

Mwanamke huyo alipigwa na butwaa kuona anakwenda Zaidi ya miezi tisa bila na dalili yoyote ya kupata uchungu wa leba.

Wasiwasi ukajipenyeza kweney nafsi yake hata Zaidi.

Akajikusanya na kunyata hadi hospitalini lakini vipimo vya madaktari vilionyesha hana ugonjwa wala mimba.

Hali hiyo ya tumbo lake kuzidi kufura kupita kiasi iliendelea kwa miaka miwili Zaidi – miezi 24!

Watu kijijini mwao walimtenga akiwemo mume wake, alilazimika kujisimamia katika hali zote yeye mwenywe, akipiga mnada kila kilichokuwa chini ya miliki yake.

Kwa mujibu wa simulizi hiyo ya haraka, Francoise alikuwa amepoteza matumaini ya kupata msaada wa matibabu ya ugonjwa wa ajabu, na alikuwa anasema maneno yake ya mwisho akitafuta mwafaka wa Amani na muumba wake, kwani tayari alikuwa ametajwa kufa mara tatu.

Afrimax kwa msaada wa watu walioona simulizi ya mwanamke huyo walisema waliweza kuchangisha kiasi cha pesa ambaco kingemsaidia kutafuta matubabu maalum.