Mwanamke wa miaka 34 aeleza sababu za kukubali kuolewa na mzee maskini wa miaka 85

“Kwangu mimi, umri ni namba tu. Kama mtu ambaye nipitia maisha na changamoto nyingi, kigezo cha umri kwa mwanamume sicho kitu ambacho kingenizuia kumpenda," mke huyo alisema.

Muhtasari

• "Mara ya kwanza nilikutana naye, ilikuwa kupitia kwa rafiki ambaye alinitajia kwamba kulikuwa na mwanamume aliyekuwa akitafuta mwanamke," alisema.

• Kwa upande wake, mzee huyo kwa jina Ephrem Kajara, alisema hana kitu chochote Zaidi ya shamba ambapo anarauka kila asubuhi kuitafutia familia yake shambani.

Wanandoa wenye pengo la umri wa zaidi ya miaka 50
Wanandoa wenye pengo la umri wa zaidi ya miaka 50
Image: screengrab

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 34 kwa jina Theodora kutoka mkoa wa Kagera nchini Tanzania amewashangaza wengi baada ya kufichua sababu zilizomvutia kwa mzee maskini zaisi mwenye umri wa miaka 84 na kukubali kuolewa naye.

Kwa kawaida, wanawake wengi hukubali kuolewa na wanaume wazee hususan kwa sababu ya mali na usalama wa kesho yao, lakini kwa Theodora, hali yake ni tofauti kwani alimkubali mzee huyo asiye na chochote cha kurithi.

Pamoja, wameishi kwa miaka 17 na wana watoto wanne.

“Mara ya kwanza nilikutana naye, ilikuwa kupitia kwa rafiki ambaye alinitajia kwamba kulikuwa na mwanamume aliyekuwa akitafuta mwanamke. Mume wangu awai alikuwa ameoa lakini wanawake wake wote walikuwa wameshindwa kupata ujauzito wake,” Theodora alianza kueleza.

“Tulikutana akanieleza jinsi alikuwa na uchu wa ujanani wa kulea watoto wake mwenyewe. Alinieleza jinsi angenipenda na mimi niliweka nadhiri ya kusimama na yeye,” aiongeza.

Kwa upande wake, mzee huyo kwa jina Ephrem Kajara, alisema hana kitu chochote Zaidi ya shamba ambapo anarauka kila asubuhi kuitafutia familia yake shambani.

“Sababu iliyonifanya kumuoa msichana huyo ni kutokana na historia mbaya ya maisha yangu ya awali katika ndoa ambapo sikuweza kujaaliwa kupata watoto. Mke wangu wa kwanza alinitoroka baada ya kushindwa kupata watoto, mke wa pili naye alianza kuonyesha tabia zisizo sawa, akitoka nje nyakati za usiku na kukimbia akipiga kelele. Baadae iligundulika kwamba alikuwa ameathirika kiakili, tukatengana,” Mzee Kajara alisimulia.

Mzee huyo alisema kwamba mke huyo alikuja kwake akiwa na mimba na akakubali kumchukua pamoja na mwanawe na kwa bahati nzuri, mwanamume aliyempa ujauzito akakataa mimba hiyo.

“Kwangu mimi, umri ni namba tu, ukweli kwamba yeye ni mzee kuniliko, nauona kama sawa tu. Kama mtu ambaye nipitia maisha na changamoto nyingi, kigezo cha umri kwa mwanamume sicho kitu ambacho kingenizuia kumpenda. Licha ya kutokuwa na vingi vya kumiliki, sisi utmeridhika na kile kidogo tunacho,” Theodora alisema.

Mke huyo alisema kwamba wazazi wake waliridhia yeye kuolewa na mzee huyo japo majirani ndio walikuwa wanaeneza uvumi na kumuapiza kwa uamuzi wake, lakini baadae walikuja kuaibika baada ya kuona ndoa yake iko imara hku ndoa zao na wapenzi wa rika lao zikiyumba.