Kutana na mwanamume ambaye hajawahi pata haja kubwa kwa miaka 13

Saidi, baba wa watoto wanne alipatwa na ugonjwa wa ajabu mwaka 2010 ambapo licha ya kula na kunywa kila siku, hajawahi pata haja kubwa na badala yake anapata haja ndogo pekee.

Muhtasari

• Hospitalini aliambiwa hana dalili za ugonjwa wowote na kulazimika kutafuta huduma za waganga wa kienyeji ambao pia hawakubaini ugonjwa.

Saidi, mwanamume aliyekosa haja kubwa kwa miaka 13.
Saidi, mwanamume aliyekosa haja kubwa kwa miaka 13.
Image: Screengrab

Hadithi ya mwanamume mmoja kwa jina Saidi kutoka nchini Rwanda imewatia wengi machungu baada ya kusimulia kwamba amekuwa na ugonjwa usiojulikana ambao umemlaza saakfuni kwa miaka 13 bila kupata haja kubwa licha ya kula na kunywa kila siku.

Saidi alikuwa dereva miaka ya nyuma kuchakarika kuitafutia familia lakini ilipofika mwaka 2010, ugonjwa wa ajabu ulimpata na kumlaza.

Kwa mujibu wa mkewe Zamuda, hali ya afya ya Saidi ilianza kama mchezo kwa kutopata haja kubwa kwa saa, siku, wiki, miezi na miaka hadi sasa ni miaka 13 na hajawahi pata haja kubwa.

“Jina langu ni Rwakagambo Saidi, nimekaa miaka 13 bila kutembelea chooni, kwa maana nyingine sijawahi pata haja kubwa licha ya kuwa nakula kila siku kama mtu yeyote lakini ikija katika suala la kuenda haja kubwa, huwa napata haja ndogo tu,” Saidi aliambia blogu ya Afromax.

Saidi alieleza kwamba alipata ugonjwa huo mapema mwaka 2010 na kuanza safari ya kutembelea vituo mbali mbali vya afya lakini vipimo vyote havikuweza kubaini ugonjwa wowote.

Alisema kwamba licha ya kutopatikana na dalili za ugonjwa wowote, lakini alikuwa anahisi uchungu, uchovu mwilini na dalili zisizoweza kuelezeka.

Saidi hakufa moyo, alitafuta huduma zingine kwa waganga wa kienyeji ambapo pia juhudi hizo hazikufua dafu.

“Nilikuwa dereva awali, nilifanya kazi kuilisha familia yangu na kila kitu kilikuwa sawa hadi pale nlipopata ugonjwa huu wa ghafla. Nilianza kumaliza muda mrefu bila kupata haja kubwa, ikawa siku na sasa ni miaka 13.”

Mkewe ambaye ni mama kwa watoto wanne alisema alimshughulikia yake yote katika hospitali mbalimbali lakini hakuweza kufaulu, akisema kwamba madaktari wengine walimwambia kuwa ni njaa tu.

“Madaktari waliniambia ni njaa tu ako nayo na anahitaji kula,” Zamuda alisema.

“Majirani walikuwa wanatusaidia mwanzoni lakini ugonjwa ulichukua muda mrefu kupona na hivyo wakasitisha misaada yao, siwezi walaumu, najua ni vigumu sana kumsaidia mtu kila siku hadi miaka 13,” Saidi aliongeza.

Sasa mwanamume huyo amesalia kwenye mkeka, kuanikwa na kuanuliwa kutoka kwa jua hadi kwenye kivuli kwa muda huo wote akisalia na tumaini finyu tu la siku moja kurejelea hali yake ya kawaida.

Kwa mujibu wa Cleveland Clinic, mtu ambaye hawezi enda haja kubwa huenda anakumbwa na ugonjwa wa kuvumbiwa baada ya mfumo wa usagaji chakula mwili unafeli kufanya kazi.