Mzee aliyekuwa akipaka avocado rangi nyeusi kuwahadaa wanunuzi apatikana (+video)

Maafisa walimpata muuzaji huyo baada ya mwanamke mmoja kulalamika aliuziwa avocado zilizopakwa rangi katika eneo la Kaharati, Muranga.

Muhtasari

•Maafisa wa usalama walimpata mzee ambaye walidai amekuwa akijihusisha na biashara ya kuwalaghai wanunuzi kwa kupaka matunda yake rangi ili kufanya yaonekane yamekomaa.

•DCC wa Murang'a South alitoa onyo kali kwa wafanyibiashara wanaojihusisha na biashara hiyo mbaya na kuwataka wajiepushe nayo.

Image: HISANI

Mamlaka ya eneo la Murang’a, mnamo Jumatatu ilimpata mfanyabiashara ambaye amekuwa akiwauzia wanunuzi parachichi zilizopakwa rangi kando ya barabara ya Murang’a - Nairobi kufuatia kilio cha hadharani cha mwanamke mmoja ambaye alikuwa mwathiriwa wa biashara hiyo haramu.

Video ya mwanamke akilalamika baada ya kuuziwa parachichi zilizopakwa rangi nyeusi katika eneo la Kaharati, kaunti ya Murang’a ilisambaa wikendi na wanamitandao wakashinikiza kukamatwa kwa wauzaji waliohusika.

Jumatatu, maafisa wa usalama wa Murang’a walimpata mzee mmoja ambaye walidai amekuwa akijihusisha na biashara mbaya ya kuwalaghai wanunuzi kwa kupaka matunda yake rangi nyeusi ili kufanya yaonekane yamekomaa.

“Tunataka Wakenya waone picha ya yule ambaye anahusika kwa haya mambo. Yule ambaye anahusika kwa kuuzia wananchi na wasafiri haya maparachichi,” DCC wa Murang’a South alisikika akisema kwenye video iliyoonekana na Radio Jambo.

Wakati akizungumza na wafanyibiashara na wakazi wengine waliojitokeza kushuhudia operesheni hiyo, ofisa huyo wa serikali alidai kuwa baadhi ya wafanyibiashara pia wamekuwa wakichoma dawa maalum kwenye ndizi ili zionekane zimeiva.

Kufuatia hayo, alitoa onyo kali kwa wafanyibiashara wanaojihusisha na biashara hiyo mbaya na kuwataka wajiepushe nayo.

“Tuko hapa tuweze kukubaliana kwamba biashara kama hiyo haiwezi kuendelea… Kwa hivyo mtachagua kama wanabiashara. Tungependa kufanya biashara ambayo ni halali na ambayo haitaumiza mwananchi na ambayo haitatarisha maisha,” alisema.

Wikendi, mwanamke mmoja Mkenya aliibua malalamishi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kununua matunda ya parachichi yaliyokuwa yamepakwa rangi rangi nyeusi ili yaonekane kama kwamba yamekomaa.

Katika video ambayo imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii, mwanamke huyo ambaye hajatambulika anaonekana akifuta rangi nyeusi iliyopakwa kwenye maparachichi na kulalamika kwamba hajui ni nini hasa kilikuwa kimepakwa kwenye matunda hayo matamu.

Alifichua kuwa baada ya kuyaweka kwa muda ili kuiva, maparachichi hayo hayakuwa yakiiva bali yalikuwa yakioza.

“Angalia nini kinafanyika kwa maparachichi haya. Kwanza utaona ni parachichi la purple kwa sababu ni Hass. Nilinunua yangu wiki moja nikaweka yaive, kukuja kuangalia nikapata hayaivi lakini sasa nimeshtuka. Kuenda kutoa maparachichi yangu yenye yananikalia kama yameiva, unaenda unapata si kuiva imeiva ni kuoza,” alisikika mwanamke huyo akilalamika kwenye video hiyo.

Mwanamke huyo alifichua kuwa alinunua maparachichi yenye sura nzuri katika eneo la Kaharati, kaunti ya Murang’a bila kujua kwamba yalikuwa yamepakwa rangi ili yaonekane ya kuvutia.

“Mimi niliona maparachichi yameiva vizuri, ya rangi ya zambarau, makubwa, hass nikasema haya siachi. Wadau kuja kuangalia nikapata maparachichi yamepakwa rangi. Ukienda kupanguza utapata yanaonekana meusi mwanzoni lakini yanakuwa kijani kibichi baada ya kupangusa,” alisema.

Alidai kuwa wafanyabiashara wanatumia mbinu hiyo kuuza matunda yao haraka sana kwa watu wanaotumia barabara ya Murang’a-Nairobi.

“Sijui hii ni rangi gani. Shida ni kwamba, hata hatujui ni kitu gani ambacho kimepakwa kwenye maparachichi haya. Tutakula mavi, tunakula sumu,” alilalamika.

Aliendelea kuonya watu dhidi ya kununua parachichi kando ya barabara ya Murang’a-Nairobi akisema kwamba wanaweza kuishia kulaghaiwa kama yeye.

“Hii ni sumu, sijui tunakoelekea kama Wakenya. Angalieni tamaa ya pesa, hivi ndivyo nilivyokuja kuona. Maparachichi yangu hayaivi, yanaoza. Unajiuliza ni rangi gani hii ambayo wameweka kwenye parachichi hizi,” mwanamke huyo alisema kabla ya kwenda kutupa matunda yaliyooza kwenye pipa la vumbi.

Wikendi, mwanamke mmoja Mkenya alibua malalamishi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kununua matunda ya parachichi yaliyokuwa yamepakwa rangi rangi nyeusi ili yaonekane kama kwamba yamekomaa.