- Tabitha Karanja anataka Lali kufunguliwa upya mashtaka
- Lali na Tecra walikuwa katika uhusiano kwa miezi 10 kabla ya kifo chake
- Familia ya Tabitha inataka kesi kufanywa Nairobi
Familia ya Tecra Muigai inamtaka mkurigenzi wa mashtaka ya umma kumshtaki upya aliyekuwa mpenzi wake Lali Omar kwa mauaji yake .
Tecra aliaga dunia mei tarehe 2 katika NAIROBI Hospital baada ya kusafirishwa kutoka Lamu baada ya kudaiwa kuanguka akiwa hotelini .Alikuwa na umri wa miaka 29 .
Lali, mwenye umri wa miaka 52 alishtakiwa kwa mauaji ya Mpenzi wake julai tarehe 13 lakini alikana mashtaka hayo .
Hata hivyo mkurugenzi wa mashtaka ya umma aliondoa mashtaka dhidi ya Omar na kuagiza uchunguzi ufanywe kuhusu kifo cha Tecra .
Katika tukio jipya sasa mamake Tecra,Tabitha Karanja amewasilisha kesi kortini akisema familia yake ilishangazwa na uamuzi wa DPP .
Karanja anamtaka DPP kuwashurutisha wachunguzi kuziba mianya katika faili ta Lali ili aweze kujibu mashtaka ya mauaji ya Tecra .
Pia amesema familia yake inataka kesi hiyo kusikizwa Nairobi ambako binti yao aliaga dunia .Amesema wahusika wote katika kesi hiyo ,familia ,wachunguzi na wataalam wengine wanaohitajika wanaishi Nairobi .
Karanja amesema familia yake inahofia usalama wao huko Lamu ambako Lali anajulikana nawatu wengi wakiwemo wahudumu wa boti .
Amemshtumu DPP kwa kutapatapa na kesi hiyo huku ikimshtumu kwa kuwa kikwazo kwa familia hiyo kupata haki .
Wachunguzi kutoka DCI wanaochunguza kifo cha Tecra wamesema Lali alikuwa mpenzi mwenye wivu na wakati mwingine alipigana na rafiki zake na watu waliodaiwa kuwa mahasimu wake. Ripoti yao imesema Tecra alikuwa mateka wa mapenzi ya Lali na alikuwa amefanya kila jitihada kujinasua .Uhusiano wao ulikuwa umedumu miezi kumi kabla ya kifo chake