- Sherehe za mwaka huu za Mashujaa zitaandaliwa Kisii
- Rais aliwashukuru viongozi wa Kisii kwa kukubali kuwa wenyeji wa sherehe za Mashujaa
- Waziri Matiang'i alikariri kujitolea kwa serikali kukamilisha miradi ya maendeleo katika eneo hilo
Rais Uhuru Kenyatta amefanya mkutano na viongozi kutoka Kisii ambapo amejadili masuala ya maendeleo ya eneo hilo . Sherehe za mwaka huu za siku ya mashujaa pia zitafanyika Kisii .
Sherehe hizo zitaandaliwa katika uwanja wa Kisii na mkutano huo ulimpa rais kenyatta fursa ya kukadiria miradi ya maendeleo pamoja na viongozi wa eneo hilo .
Wakiongozwa na magavana James Ongwae wa Kisii na John Nyangarama wa Nyamira viongozi hao walizungumza na rais Kuhusu miradi mbali mbali ya barabara ,elimu na soko kwa mazo ya watu wao .
Katika waraka maalum uliowasilishwa kwa rais na gavana Ongwae viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa muungano wa watalaam kutoka Kisii John Simba na mwenyekiti baraza la wazee wa jamii hiyo James Matundura ,walimshukuru rais kwa mipango kadhaa ya amendeleo inayoendeshwa na serikali kuu .
Walizitaja barabara kadhaa ,miradi ya maji ,hospitali na masoko ya daraja mbili na Nyakoe kama baadhi ya miradi inayosaidia kuboresha hali ya aisha ya wakaazi .
Wakati huo huo viongozi hao walimtaka rais kuhakikisha kwamba miradi inayoendeshwa kwa sasa inatamatishwa kwa wakati . Rais alikuwa na mawaziri Fred Matiangi wa usalama wa ndani , James Macharia wa uchukuzi na Mutahi Kagwe wa Afya wakati wa mkutano huo .