Sakata ya DJ Mo na Margaret Wanyama inatishia ndoa ya Size 8

Nyani haoni Kundule: Kinaya cha Betty Bayo kumpa ushauri wa ndoa Size 8!

Size 8 amesema ataipigania ndoa yake na DJ Mo

Muhtasari
  •  Size 8 anapigania ndoa yake baada ya sakata kumkumba DJ Mo na mwanamke mwingine 
  •  Betty Bayo alitalakiana na mume wake Pastor Kanyari na maajuzi wametupiana cheche za maneno mtandoani 
  • Wengi wanahoji iwapo 'ushauri' wake kwa Size 8 ni  wa kweli ama  wa kudakia masafa ya mitandao ya kijamii 

 

Betty Bayo,Kushoto na DJ Mo na Size 8

Kuna msemo kwamba Uamuzi ndio dawa pekee unayofaa kumeza bila ushauri wa daktari .

Kama msemo huo , wakati unapopatwa na matatizo  unahitaji watu kukupa ushauri na mitazamo lakini kitu kikubwa kwako huwa kujifanyia uamuzi mwenyewe

 Ingawaje kila mtu ana haki ya kutoa ushauri kwa mwenzake , msanii wa  nyimboz za Gospel amewashangaza wengi kwa kujitokeza kumpa ushauri Size 8 ambaye anapitia mengi katika ndoa yake na DJ Mo baada ya kutolewa madai kwamba DJ Mo alikuwa akishiriki mahusiano ya nje ya ndoa .

 Mwanamke mmoja aliyejitambua kama Margaret Wanyama alijitokeza kufichua kwamba amekuw ana uhusiano wa kimapenzi na DJ Mo ,a kumuacha msanii Size 8 katika msururu wa maombi ili kuiokoa ndoa yake .

Margaret Wanyama ,mwanamke aliyedai kuwa katika uhusiano na DJ Mo

 Lakini ,kando na kuwa na haki yake ya kutoa ushauri kwa Size 8 , Betty Bayo hangejitokeza hasa baada ya historia yake inayojulikana ya kuvunjika kwa ndoa yake na pia kwamba haypupo katika mahusiano yanayojulikana kwa sasa

 Betty alikuwa mkewe Pastor Kanyari  na alimuacha baada ya mhubiri huyo kutibuliwa kwa  kufanya ‘miujiza’ feki. Watu wengi sasa wanashangaa ni vipi Bayo atajipa jukumu la kumpa Size 8 suahuri ilhali hakuweza kuipigania nda yake na Pastor Kanyari .

 Iwapo kweli Betty  ni mkweli bai pia angemsamehe mume wake ikizingtiwa kwamba hapakuwa na madai ya usinzi katika ndoa yake

 Betty pia hajakuwa akitoa taswira ya kuvutia mtandaoni kwani baadahi ya posti zake zimefichua kwamba anatamani sana kuolewa ama kupendwa tena .

 Kuna madai kwamba huenda hatua yake ya kujifanya kumpa Sze 8 ushauri ililenga tu kusalia katika ndimi za mitandao ya kijamii .