Shtaka la Mauji

Jumwa Mashakani:DPP aidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya mbunge Aisha Jumwa

Jumwa yupo katika mrengo wa DP Ruto baada ya kukiasi chama cha ODM

Muhtasari
  • Tukio lilitokea mwaka jana wakati Jumwa alipovamia mkutano wa ODM 
  • Mwanamme mmoja alipigwa risasi katika patashika iliyozuka 

 

Mbunge Aisha Jumwa,
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa Mbunge Aisha Jumwa,

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ameidhinisha kushtakiwa kwa mbunge wa Malindi  Aisha Jumwa kwa mauaji ya mwanamme mmoja  wakati wa ghasia zilizozuka kwenye uchaguzi mdogo wa  wadi ya Ganda mwaka uliopita .

 Mwanamme huyo alipigwa risasi wakati wa patashika iliyozuka  huko Malindi oktoba mwaka jana  wakati wafuasi wa Jumwa aaliposhambuliana na wafuasi wa chama cha ODM

 Kisa hicho kilifanyika wakati Jumwa  alipovamia mkutano wa ODM  akitaka kujua kilichokuwa kikifanyika  wakati huo wa usiku  baada ya muda wa kampeini kutamatika . Maafisa wa ODM  walisisitiza kwamba mkutano huo ulikuwa wa mafunzo kwa maajenti wa chama cha ODM .

 Jumwa anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa kiakili  wiki ijayo kabla ya kufikishwa kortini kujibu mashtaka . Mwanamme aliyeua katika tukio hilo alikuwa jamaa ya mgombeaji wa  ODM Katika uchaguzi huo mdogo Reuben Katana ambaye aliibuka mshindi