Masaibu ya Pesa

Kasisi John Pesa wa ‘Solomon aliua Goliath’ asema maisha yake yamo hatarini baada ya ziara ya Sugoi

Amedai kupokea vitisho vya kuuawa

Muhtasari

 

  • Kasisi Pesa amedai kupewa 10,000
  • Amesema yuko tayari 'kufa' baada ya kupkea vitisho 
  • Alikuwa katika ujumbe wa viongozi wa makanisa waliomtembelea Ruto, Sugoi 

 

Kasisi John Pesa

Kasisi John Pesa ambaye mahubiri yake yalihusisha  usemo kwamba Solomon ndye aliyemua Goliath akiwa katika ziara   ya viongozi wa kidini kutoka Nyanza kwa naibu wa rais William Ruto huko Sugoi amedai kwamba maisha yake yamo hatarini

Pesa  ambaye alilenga kumhusisha Ruto na David  ambaye alimwuua Goliath katika Biblia  aliteleeza na kusema kwamba ni Solomon ndiye aliyemua Goliath hatua iliyozua sana mhemko katika mitandao ya kijamii na kila aliyekuwa akitazama mahubiri yake .

"Mimi ni mzee sana..sikumanisha nilivyosema.  Nasikitika kwamba watu wangali  wanaendeleza ptyovu huo kuhusu nilichosema’ amesema Pesa

 

 Pia amedai kwamba maisha yake yamo hatarini baada ya ziara yake kumuona Ruto . Mhubiri huyo amesema tangu walipomtembelea Ruto  amekuwa akipokea jumbe za vitisho huku baadhi ya watu wakija kwake awape pesa ambazo wanasema alipewa na Ruto

John Pesa akiwa na Naibu wa Rais William Ruto

 Amesema ameripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Kondele huko Kisumu .Pesa amekanusha kupewa fedha wakati wa ziara hiyo

"Ruto ni hasla na hana pesa’ amesema

 Hata hivyo kulingana na gazeti la Taifa Leo  kassi huyo alidai kupewa shilingi elfu kumi pekee wakati wa ziara hiyo nyumbani kwa Ruto

 Ameliambia gazeti hilo kwamba kati ya pesa hizo alitumia shilingi 6000 kuweka mafuta kwenye magari yake mawili kwa safari ya kutoka Kisumu hadi sugoi na kusalia na shilingi 4000 pekee .

 Amedai kwamba  aligundua kwamba viongozi wengine wa makanisa waliokuwa katika ujumbe huo walipewa kiasi cha juu cha pesa kuliko shilingi elfu kumi ambazo yeye alipewa .

‘ Hilo linafaa kulaaniwa sana ,pesa kama hizo hazifai kupewa watu kwa njia ya ubaguzi’ amesema Pesa