- Amesema katiba ya 2010 iliwapa polisi kuhudumu bila muingilio wowote wa kisiasa .
- Amesema katika mapendekezo ya BBI senate imepunguziwa nguvu za kuamua kuhusu raslima za kaunti na matumizi yake
- Timu haziwezi kumchagua refarii -Ruto
Naibu Wa rais William Ruto siku ya jumatatu ameeleza pingamzi yake kuhusu baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya BBI jinsi ilivyo sasa akisema mambo hayo yanafaa kurekebishwa na wakenya wote kupewa fursa ya kutoa michango yao ili kuiboresha hata Zaidi .
Idara ya mahakama
Ruto amesema kwamba pendekezo la kuundwa kwa afisi ya kutoa malalamishi kuhusu idara ya mahakama ambayo mshikilizi wake atateuliwa na rais ni jambo am,balo litavuruga uhuru wa idara hiyo . Ruto amesema hiyo inaweza kulirejesha taifa katika siku za kale ambapo maamuzi ya majaji yaliamuliwa na rais kupitia simu .
" Tunafaa kuanza kuitumia hazina yay a idara ya mahakama ili iweze kuwaajiri majaji zaidi na kujenga korti katika kila sehemu za nchi kuwahudumia wakeny’ amesema Ruto .
Tume ya uchaguzi
Kuhusu pendekezo la makamishna wa uchaguzi kuteuliwa na vyama vya kisiasa Ruto amesema hatua hiyo ni kama kuzipa baadhi ya timu maamlaka ya kumteua refarii katika michuano
“ swali ambalo najiuliza ni je mchuano kama huo kutakuwa na haki ?’
Kuhusu kuzuia mshindi katika uchaguzi kuchukua yote Ruto alishangaa jinsi mapendekezo hayo yatakavyozuia hilo ilhali rais ,naibu wake na waziri mkuu na manaibu wake watakuwa kutoka upande mmoja wa kisiasa .
Huduma ya polisi
Ruto, alizungumza kuhusu huduma ya polisi na kuundwa kwa baraza la polisi .amesema katiba ya 2010 iliwapa polisi kuhudumu bila muingilio wowote wa kisiasa .
‘Pendekezo la kuwa na baraza la polisi litakaloonozwa na waziri ni kuvuruga uhuru wa polisi’
Ugatuzi
Kuhusu kuongezwa kwa mgao wa fedha za kauti kutoka asilimia 15 hai 35 Ruto amesema hilo linafaa kuambatana na bunge la senate lenye nguvu . Amesema katika mapendekezo ya BBI senate imepunguziwa nguvu za kuamua kuhusu raslima za kaunti na matumizi yake . Pia amepinga kuondolewa kwa nafasi ya mwakilishi wa akina mama kutoka bunge . Amesema pia kwamba suala la uundaji wa nafasi za ajira na kuboresha biashara ndogo ndoo na za kadri ni jambo linalofaa kutathminiwa upya
Hotuba ya Ruto kuhusu masuala hayo ya BBI haikuwapendeza baadhi ya wajumbe katika ukumbi wa Bomas lakini naibu wa rais alisema ana haki ya kuhoji na kuyazua katika mjadala kuhusu njia za kuboresha ripoti hiyo .Baadhi ya wajumbe walianza kumkemea Ruto kwa kelele na akatamatisha hotuba yake kwa kumualika rais Uhuru Kenyatta ambaye alionekana kuiunga mkono ripoti hiyo jinsi ilivyo akisema masuala mengine yanayoonekana kama udhaifu wa ripoti hyo yanaweza kushughulikia mchakato mzima ukiendelea .