Mpenzi wa Marehemu ajitokeza

Mwanamke ashtaki kuzuia kuzikwa kwa mbunge Murunga akisema ana watoto naye

Agnes amesema ana watoto wawili na marehemu Murunga

Muhtasari

 

  •  Agnes Wangui anataka vipimo vya DNA kufanywa ili kuthibitisha kwamba baba ya watoto wake ni Mbunge Murunga 
  •  Anataka kuhusishwa katika mipango ya mazishi ya mbunge huyo wa zamani wa Matungu 
  • Amesema alianza uhusiano  na marehemu mwaka wa 2013

 

Justus Murunga

 Mwanamke anayedai kwamba ni mpenzi wa marehemu mbunge wa Matungu  Justus Murunga  amewasilisha kesi kortini ili kuzuia  kuzikwa kwa mbunge huyo .

 Kupitia wakili wake Danstan Omari ,Agnes Wangui wanawtaak wajane wawili wa Murunga  - Christabel  na Grace  na hifadhi ya maiti ya Lee  wazuiwe  dhidi ya kumzika mbunge huyo .

 Pia anataka mahakama kutoa ruhusa ya kuchukuliwa kwa sampuli za DNA za mbunge huyo na watoto wa Agnes ili kuthibitisha kwamba watoto hao ni wa Murunga .

 Pia anataka mwili wa mbunge  huyo kuhifadhiwa Lee hadi wakati sampuli ya DNA  itakapotolewa  pakiwepo mwanapatholojia  aliye na leseni ambaye atateuliwa na pande zote mbili .

Agnes,  amesema watoto wake wawili ni wa marehemu mbunge huyo . Amesema anahofia wajane wake wawili wanaweza kupanga njama  ya kumfungia nje pamoja na wanawake katika mipango ya kumzika Murunga .

 Kupitia waraka kwa mahakama amesema amemjua mbunge huyo kwa mika saba tangu mwaka wa 2013  alipokuwa msimamizi katika shamba la Embakasi   na  yeye alipokuwa mfanyibiashara  katika eneo la Ruai .

 Agnes amesema baada ya kuanza kwa uhusiano wao wa kimapenzi na kuwapata watoto wawili  ,Murunga alimkodishia nyumba katika mta wa Ruai.Uhusiano wao ulianza kuvurugika mwaka wa 2017 baada ya mbunge huyo kushinda kiti cha ubunge cha Matungu