Mkasa wa Boti

Ruto azifariji familia ziliwapoteza watu 10 katika ajali ya boti huko Usenge

Watu kumi wamefariki

Muhtasari
  • Wenyeji wanashirikiana na wavuvi kutafuta miili zaidi 
  •  Mwili wa mwanamke mmoja umeshapatikana 
  • Watu kumi akiwemo mtoto wameokolewa 

 

Naibu wa rais William Ruto amezifariji familia zilizwapoteza watu 10 baada ya boti waliomokuwa wakisafiria kuzama katika  ziwa Victoria .

" Ni jambo la kuhuzunisha kwamba tumewapoteza  wakenya  katika ajali ya boti ziwani Victoria .rambi rambi zangu ziwaendee watu wa familia zilizowapoteza wapendwa wao huko Siaya’ amesema Ruto

 Mwenyekiti wa usimamizi wa Ufuo katika eneo ambako ajali hiyo iliyokea  Elly Odhiambo Masinde amesema boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 20  ilipozama majini kwa sababu ya upepo mkali .

 Amesema watu kumi walikufa maji ilhali wengine kumi waliokolewa wakiwemo watu 9 wazima na mtoto mmoja  aliyeokolewa na wavuvi .

 Naibu wa chifu wa  Got Agulu Fredrick Ochieng  amesema shughuli ya kuiondoa miili hiyo majini inaendlea .Ameitaka serikali kuwapa msaada katika opareshei hiyo .

 Mwili wa mwanamme mmoja umeshapatikana hadi  kufikia sasa . oparesheni hiyo inaendeshwa na wavuvi wa eneo hilo ,kundi la usimamizi wa ufuo na  maafisa wa  Kenya Coast Guard

 Ripoti zasema maafisa wa usalama wa majini wanawasiliana na Uganda ili kusafirisha mwili kwa marehemu hadi Uganda . Gavana wa Siaya Cornel Rasanga  pia ametuma risala za rambi rambi kwa  familia zilipatwa na mkasa huo .Rasanga ameahidi kuzisaidia familia ziliwapoteza wapendwa wao na zile ambazo miili ya jamaa zao haijapatikana .