sakata ya wizi wa watoto

Afisa mkuu mtendaji wa Hospitali ya Mama Lucy na watu wengine 2 kuzuiliwa kwa siku 2

sakata hiyo ilifichuliwa na makala ya BBC

 

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya Mama Lucy  na watu wengine wawili  ambao wanashtumiwa kwa sakata ya uuzaji wa watoto watasalia rumande kwa siku  ili kuruhusu uchunguzi dhidi yao kufanyika .

 Afia huyo mkuu Emma Mutio na  Makallah Fred na Regina Musembi waliwekwa rumande baada ya agizo la  hakimu Bernad Ochoi  .

 Katika uamuzi wake Ochoi  amesema maafisa wa uchunguzi wako sawa kuwa na hofu kuhusu uwezekano wa  washukiwa kuvuruga ushahidi wa stakabadhi dhidi yao

Makallah  alifichuliwa katika uchunguzi uliofanywa na BBC alipokuwa akijadiliana na mwanahabari wa BBC kuhusu mpango wa kumuuza mtoto ambaye aliyekuwa ameachwa katika hospitali ya Mama Lucy .

 Korti imewaweka rumande watatu hao katika kituo cha polisi cha kileleshwa  hadi novemba tarehe 23 wakati kesi hiyo itakapotajwa .