BBI imekosa kutamba Mt. Kenya - Kang'ata

Muhtasari

• Katika barua kwa Rais iliyofikia Star, mbunge huyo anasema amegundua kwamba BBI haipendwi Mlima Kenya.

• Wengi wanapinga kupanuliwa kwa serikali.

UKWELI USEMWE: Kiranja wa wengi katika Seneti Irungu Kang'ata Picha: MAKTABA
UKWELI USEMWE: Kiranja wa wengi katika Seneti Irungu Kang'ata Picha: MAKTABA

Huenda kura ya maoni ya BBI ikakosa kupata uungwaji mkono katika eneo la Mlima Kenya ikiwa Rais Uhuru Kenyatta na mshirika wake wa ‘handshake’ Raila Odinga hawatabadilisha mkakati wao.

Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata ambaye pia ni kiranja wa wengi katika seneti ametoa onyo mapema kwa Kenyatta kwamba anakabiliwa na hatari ya kuachwa mpweke katika ngome yake ya mlima Kenya.

Katika barua ya ujasiri kwa Rais iliyofikia Star, mbunge huyo anasema amegundua kwamba BBI haipendwi Mlima Kenya.

Alitaja upinzani dhidi ya kupanuliwa kwa serikali na kushirikishwa kwa utawala wa mkoa na hatua ya wabunge wa zamani kuongoza kampeni za kuipigia debe BBI kama sababu kuu zanazofanya ikataliwe.

Seneta alisema jukumu la machifu na wasimamizi wa kaunti - na mbinu zingine za kulazimisha katika uhamasishaji wa BBI ni changamoto katika eneo hilo.

"Wacha tusisitize nguvu taratibu na ushawishi. Kwa mtazamo wangu mnyenyekevu, juhudi za utawala wa mkoa katika mchakato wa BBI hazifai kuonekana, ” amwambia Kenyatta.

Kang’ata, ambaye alichukua majukumu ya kiranja wa seneti kutoka kwa Seneta wa Nakuru Susan Kihika, alisema kuhusika kwa maafisa wa serikali ya kitaifa kunaweza kuchukuliwa kama "matumizi ya nguvu na serikali kuwalazimisha raia wake kuidhinisha BBI."

Kiranja huyo wa Seneti alisema BBI inakabiliwa na tishio kuangushwa  ikiwa Rais hatachukua hatua za haraka za kuinadi.

Anamtaka rais Kenyatta kuchukua jukumu la kuipigia debe  BBI katika eneo la Mt Kenya, akisema kampeni ya sasa haina uratibu.

Kang’ata anamtaka rais Uhuru Kenyatta kutumia mswada mpya wa chai na juhudi za kufufua kilimo cha kahawa katika eneo hilo kuuza BBI.

Mwanasiasa huyo alionya "kura ya HAPANA katika eneo hilo hayiwezi kusisitizwa zaidi."

"Ninaomba tufanye juhudi za haraka za kurekebisha dhana kama hiyo," Seneta anasema katika barua hiyo ya kurasa sita.

Anazidi kusema kuwa matokeo ya mgombeaji wa Jubilee katika kinyang'anyiro cha ugavana wa Nairobi pia utakuwa na athiri sana kwa BBI.

Anataka Rais aingilie kati, kama jambo la dharura, na atulize malumbano katika Jubilee ambayo yanaathiri BBI.

"Jitihada zinahitajika kufanywa kuwakusanya wabunge wote wa kutoka kila eneo bila kujali mirengo yao ya kisiasa kwa sababu hii."

Kang’ata amependekeza kura ya maoni yenye maswali mbali mbali ili kuzuia uwezekano wa kukataliwa kabisa kwa mapendekezo ya BBI.

Walakini, anakataa pendekezo la Naibu Rais William Ruto na wafuasi wake kwamba kura ya maoni ifanyike pamoja na uchaguzi wa 2022.

Kang’ata anadai kwamba wabunge wa ‘Kieleweke’ ambao wamesimama na Rais kwa hali na mali wamewekwa pembeni katika mchakato huo.