Biden aidhinishwa kushinda uchaguzi wa urais na bunge

Muhtasari

  • Bunge la Congres limemuidhinisha Joe Biden na Kamala Hariss kama rais mtarajiwa na makamu wake wa Marekani.

  • Shughuli za bunge zilikatizwa siku ya Jumatano wakati wafuasi wa rais Trump walipovamia jumba la Capitol Hill.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden

Bunge la Congres limemuidhinisha Joe Biden na Kamala Hariss kama rais mtarajiwa na makamu wake wa Marekani.

Bunge hilo liliwaidhinisha wawili hao kwa kura 282 huku wabunge 138 wakipiga kura ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania.

Bunge la seneti lilikataa pingamizi kama hiyo.

Kura za wajumbe zilithibitishwa baada ya mabunge yote mawili lile la uwakilishi na lile la seneti kukataa pingamizi kuhusu kura zilizopigwa katika vituo vya jimbo la Pennsylvania na Arizona.

Shughuli za bunge zilikatizwa siku ya Jumatano wakati wafuasi wa rais Trump walipovamia jumba la Capitol Hill.

Shughuli baadaye zilirejea na kuendelea usiku kucha baada ya waandamanji hao kutolewa.

Bunge la uwakilishi pamoja na lile la Seneti litaendelea kuhesabu kura za wajumbe zilizosalia ili kumuidhinisha Joe Biden kuwa rais mtarajiwa wa Marekani.