Mauaji ya Kiambu, uchunguzi waonyesha muuaji alikuwa na ustadi wa kuua

Muhtasari

  • Upasuaji wa miili ulionyesha kuwa majeraha ya kudungwa kwenye miili yalipimwa kati ya milimita tatu hadi nne.

  • Kulingana na majeraha inaonekana muuaji alikuwa na hasira sana na babake na kakake.

Maafisa wa DCI wabeba sampuli za miili ya wahasiriwa wa mauaji ya watu 5 katika kaunti ya Kiambu.
Maafisa wa DCI wabeba sampuli za miili ya wahasiriwa wa mauaji ya watu 5 katika kaunti ya Kiambu.
Image: ANDREW KASUKU

Nicholas Warunge, mkewe, mtoto wake, mpwa wake na mfanyakazi wao waliuawa kwa usahihi wa ustadi, miili yao ilikuwa na majeraha sawa kwa vipimo na kina, ripoti ya uchunguzi wa mwili ilionesha.

Upasuaji wa miili uliofanywa Jumatatu ulionyesha kuwa majeraha ya kudungwa kwenye miili yalipimwa kati ya milimita tatu hadi nne.

Mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor alisema kiwango cha kufanana kwa majeraha ni ishara kwamba aliyetekeza mauaji hayo alikuwa mtu mmoja au "ikiwa walikuwa watu tofauti, basi walitumia silaha moja ya mauaji."

Mwana wa kwanza wa marehemu Warunge Lawrence Simon Warunge alikiri kutekeleza mauaji hayo.

Ripoti ya uchunguzi wa maiti ilionyesha kuwa muuaji alikuwa na hasira kali zaidi kwa baba na kakake kwani miili yao ilikuwa na majeraha mengi.

“Mwili wa baba ulikuwa na idadi kubwa ya majeraha ya kudungwa na sawa na mwili wa mwanawe wa kiume. Wote wawili walikuwa wamekatwa shingo na vichwa vyao kung’olewa, ”alisema.

"Majeraha katika mwili wa baba na mwanawe wa kiume yanaonyesha kuwa muuaji alifurahia kitendo chake au alikuwa na hasira wakati akitekeleza uhalifu huo," Oduor aliongeza.

Ni mama na kaka mdogo ambao walionekana kujaribu kukabiliana na muuaji, alielezea. Wote wawili walikuwa wamevunjika mikono na majeraha ya kudungwa, ishara kwamba walikuwa wakiinua mikono yao kujikinga wasigongwe na silaha butu na kifaa chenye ncha kali.

Matokeo ya uchunguzi wa mfanyikazi mwili wa mfanyikazi yalionyesha pia kwamba aligongwa na kifaa kwa kichwa  kando kando na ishara za kudungwa kisu.

"Inaonekana mshukiwa alimkuta mwathiriwa akiwa amelala. Hakujitahidi sana kujikinga,” mwanapatholojia aliongezea.

Lawrence, 23, alifikishwa katika korti ya Kiambu Jumatatu kwa ajili ya kusikilizwa ombi la waendesha mashtaka kutaka yeye na rafiki yake wa kike wazuiliwe kwa siku 14.

Korti iliruhusu ombi hilo kuwezesha wachunguzi kufanya uchunguzi kamili, pamoja na upimaji wa DNA na kulinganisha na pia tathmini ya akili ya mshukiwa.