Muhtasari
- Raab baadaye jumatano atakutana na waziri wa afya wa Kenya Muytahi Kagwe ili kujadiliana kuhusu jinsi Kenya itakavyopata chanjo ya Corona Oxford-Astrazeneca .
- Pia atakagua majaribio ya utoaji wa chanjo hiyo huo Kilifi . Raab yuko nchini kwa ziara ya siku moja .
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab ametangaza kwamba nchi yake itaipa Kenya pauni milioni 9 ili kupiga jeki vita vyake dhidi ya kundi la kigaidi la al shabaab .
Kenya pia itanufaika na pauni milioni 48 za kuisadia kufadhli miradi ya kupmabana na mabadiliko ya hali ya anga hasa katika maeneo ambako athari za mageuzi ya hali ya anga yameziathiri jamii kwa kusababisha kiangazi na mafuriko .
Raab baadaye jumatano atakutana na waziri wa afya wa Kenya Muytahi Kagwe ili kujadiliana kuhusu jinsi Kenya itakavyopata chanjo ya Corona Oxford-Astrazeneca .
Pia atakagua majaribio ya utoaji wa chanjo hiyo huo Kilifi . Raab yuko nchini kwa ziara ya siku moja .