- WHO pia imesema watu ambao miili yao inaweza kujibu vibaya viungo vyovyote vya chanjo hiyo hawafai kuitumia chanjo hiyo au chanjo yoyote ya mRNA.
- Chanjo hiyo pia haifai kupewa watu walio chini ya umri wa miaka 18 hadi matokeo ya utafiti Zaidi yatolewe .
Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa chanjo ya Corona ya moderna haifai kupewa wanawake walio wajawazito .
Hakuna majaribio ya chanjo hiyo yaliofanywa kwa wanawake walio na uja uzito na hayatarajiwi kufanywa hadi robo ya kwanza ya mwaka wa 2021 ,WHO imesema
" Ingawaje uja uzito unawaeka hatarini wanawake kukumbwa na covid 19 matumizi ya chanjo hii kwa wanaotarajia kupata watoto hayafai ..’ WHO imesema kupitia taarifa .
Mkurugenzi wa chanjo Kate O'Brien amesisitiza kwamba majaribio ya chanjo ya Moderna kwa wanawake waja wazito yanahitajika kwa wanawake walio na mimba .
" Hakuna sababu ya kufikiria kwamba kuna tatizo la kuwa na uja uzito tunakiri tu kwamba maelezo hayapa kwa sasa’ amesema
WHO pia imesema watu ambao miili yao inaweza kujibu vibaya viungo vyovyote vya chanjo hiyo hawafai kuitumia chanjo hiyo au chanjo yoyote ya mRNA.
Chanjo hiyo pia haifai kupewa watu walio chini ya umri wa miaka 18 hadi matokeo ya utafiti Zaidi yatolewe .
Siku ya jumatatu Moderna Inc ilisema chanjo yake inatoa chembe za kukabiliana na virusi vya Corona dhidi ya aina mpya ya virusi vya ugonjwa huo vilivyogundulika nchini Uingereza na Afrika Kusini .
Dozi mbili ya Moderna inatarajiwa kukabiliana na aina yoyote itakayochipuka ya virusi hivyo ,kampuni hiyo imesema .